Hakuna chakula cha msaada -Magufuli


Rais John Magufuli akikata utepe akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka pamoja na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa kuashiria ufunguzi wa barabara ya Bariadi-Lamadi yenye kilometa 71.8. (Picha na Ikulu).
RAIS John Magufuli amesema inawezekana asiwe mwanasiasa mzuri, lakini siku moja atakumbukwa kwa mambo ambayo anayafanya, kwa sababu dhamira yake ni nzuri katika kusimamia ubadhirifu wa fedha za umma na kusimamia miradi ya maendeleo ili watanzania wote wanufaike.

Pia amesisitiza kuwa serikali haitatoa chakula cha msaada kwa wananchi. Aidha, katika kusimamia kauli zake mkoani Simiyu, Rais Magufuli ameagiza hospitali ya rufaa ya mkoa wa Simiyu ambayo aliweka jiwe la msingi, ujenzi wake jana kujengwa kwa Sh bilioni 10 na kukataa kiwango kilichokuwa kimekadiriwa cha Sh bilioni 46.

Rais Magufuli alitoa kauli hiyo jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Somanda wilayani Bariadi, kabla ya kwenda kuzindua ujenzi wa barabara.

Awali Rais alikuwa na mikutano mingine katika vijiji vya Nyashimo, Masanzakona, Lamadi na Nyamikoma wilayani Busega mkoani Simiyu katika siku ya kwanza ya ziara yake mkoani humo.

“Nimeweka jiwe la msingi katika ujenzi wa hospitali, ujenzi wake wamesema ni Shilingi bilioni 46, nimesema kitu hicho hakiwezekani, tena wamekosea sana kuniita mimi kuja kuweka jiwe la msingi,” alisema Rais Magufuli.

No comments:

Post a Comment