DAR ES SALAAM: MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu inatarajiwa kutoa uamuzi wa kumwachia ama kutomwachia huru mke wa marehemu bilionea Erasto Msuya aitwaye Miriam Mrita (41) na mwenzake ambaye ni mfanyabiashara, Revocatus Muyela (40), wanaotetewa na mawakili Peter Kibatala na John Mallya ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Januari 23 mwaka huu.
Uamuzi huo ulitolewa leo mahakamani hapo kutokana na upande wa serikali kushindwa kubadilisha hati ya mashtaka ya kesi hiyo ndani ya siku mbili kama ilivyoamliwa Januari 9, mwaka huu.
Januari 9, 2017 Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa, aliuamuru upande wa serikali kubadilisha hati ya mashitaka ndani ya siku mbili ambapo alisema uamuzi huo unatokana na kupitia hoja za pande zote mbili na kubaini kuwa hati ya mashitaka ilikuwa na mapungufu mawili likiwemo la kutoonyesha kama kuna mtu ambaye amesababisha kifo kwa mtu mwingine.
No comments:
Post a Comment