BINTI AMEFANYIWA UPASUAJI MARA TISA (9) LAKINI BADO, WATANZANIA MSAIDIENI HUYU MWENZETU

 
Habari Ndugu Mtanzania Mzalendo,Kwa majina Naitwa Exaud Mtei, Mwandishi wa Habari nchini Tanzania, kwa Masikitiko makubwa Imebidi niwe Balozi wa Kusambaza Ujumbe huu ambao nimeupata kutoka kwa mwalimu wa shule ya Kawe Ukwamani akinieleza Kuhusu maisha ya mwanafunzi wake wa Kidato cha Nne ambaye anashindwa kundelea na masomo kutokana na Matatizo yanayomkumba-

HUU NI UJUMBE WA MWALIMU HUYO--
HABARI KAKA-Kuna mwanafunzi wangu anaitwa Mariam Ibrahimu Mwema wa shule ya sekondari Kawe ukwamani kidato cha 4 mwenye umri wa miaka 16 tu ana matatizo makubwa ya tumbo. Alifanyiiwa opereshen ya kwanza  akiwa darasa la 3. Baadae  upasuaj uliendelea takriban mara 9.    
                   
Hali yake kiafya imezorota tena baada ya kuimarika katika miezi 2 Iliyopita kufuayia operation aliyofanyiwa pale Muhimbili .Ilikuwa ni operation ya kumi kwa huyu binti mwenye umri chini ya miaka 18                       
Dogo kwa sasa ni wa kutapika tu, tumbo limevimba tena na kitu kiumizacho zaidi ni kuwa FAMILIA YAKE IPO TAABANI KIUCHUMI KWA SASA...!                     Anaumwa kiukweli dogo hata kukaa hawez..!             

No comments:

Post a Comment