Aliyekuwa Mwendesha Mashtaka wa juu jijini New York, amevieleza vyombo vya habari nchini humo kuwa alifukuzwa kazi na Rais Donald Trump baada ya kupokea simu kadhaa zisizokuwa za kawaida kutoka kwa Rais huyo wa Marekani.
Preet Bharara aliambia shirika la ABC wiki hii kuwa alihisi simu hizo kutoka kwa Rais Trump zilikuwa zimevuka mipaka ya kawaida inayotenganisha ofisi ya rais na uchunguzi huru wa uhalifu.
Bharara amesema kuwa alifukuzwa kazi baada ya kukataa kupokea simu ya tatu ya Trump.
Ikulu ya White House haijajibu madai hayo ya Bharara.
Bharara ambaye aliteuliwa na Obama na kuhudumu eneo la Manhattan, amesema ilionekana kuwa Trump alijaribu kujenga uhusiano fulani baada ya wawili hao kukutana mwaka 2016.
"Rais Obama hakunipigia simu hata mara moja katika kipindi cha miaka saba na nusu.” amesema.
No comments:
Post a Comment