KUTANA NA 'TYRESE' WA TANZANIA AITWAYE BANYE


Elias Banyenza ndio jina alilopewa na wazazi wake, lakini unafahamika na wengi kwa jina la Banye. Anapenda kuimba na RnB ndio muziki ana unaoupenda zaidi. Banye alianza kuimba akiwa Sunday Schools na Talent Shows lakini alivutiwa zaidi na Mwanamziki Tyrese tangu alipomuona mara ya kwanza kwenye Tangazo la Coca-Cola la mwaka 1986 na kujaribu kumfuatisha jinsi alivyoimba kila mara lile Tangazo lilipopita. 
Watu wengi wakimuona kwa mara ya kwanza huwa wanahisi kama waliwahi kumuona sehemu nahisi hii ni kwasababu waliwahi kuomuona kwenye sehemu zifuatazo:- Mwaka 2014/2015 alikuwa miongoni mwa wawashiriki 6 (Damian Soul,Grace Matata,Eli Daddy, Rogers Lucas, Myra) waliowakilisha Tanzania kwenye shindano la kuimba la Maisha Superstar nchini Kenya, kipindi hicho cha Tv kilirushwa na Maisha Magic ambapo walienda kushindana na washiriki wengine 12 kutoka nchi tofauti tofauti za Africa Mashariki, walisimamiwa na Shaa, AY(Tanzania), Jose Chameleon, Maurice Kirya (Uganda),Nameless, King Kaka(Kenya) na Music Director alikuwa Eric Wanaina. 

No comments:

Post a Comment