POLISI WAMALIZA KUMPEKUA LISSU NYUMBANI KWAKE

Jeshi la Polisi limemaliza upekuzi waliokuwa wanafanya nyumbani kwa Mwanasheria Mkuu wa Chadema Tundu Lissu wanaelekea Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.
Taarifa ya msemaji wa Chadema Tumaini Makene amesema Lissu anapelekwa polisi kwa ajili ya taratibu zingine za kisheria kuendelea ikiwa ni pamoja na dhamana yake ambayo kisheria iko wazi.
Amesema upekuzi uliofanyika ulihusu makosa mawili anayotuhumiwa nayo ya kumkashifu rais na Uchochezi kuhusu kushikiliwa ndege ya Tanzania aina ya Bombardier Q400 huko nchini Canada.

Chanzo: Mwananchi

No comments:

Post a Comment