JAMES OLOLO ANASHIKILIWA NA POLISI UBELIGIJI KWA KUMUUA MKEWE ELIZABETH WAFULA

James Ololo akiwa na mkewe Elizabeth Wafala enzi za uhai wake.

James Ololo Mkenya wa miaka 55 anayeishi Ubeligiji anashikiliwa na polisi wa nchi hiyo baada ya kumuua mkewe amabye pia ni Mkenya Elizabeth Wafula.

Gazeti la Ubeligiji HLN,  limeripoti James Ololo alikwenda nyumbani kwa mkewe Elizabeth ambaye walikua hawaishi pamoja na kumwomba afute kesi ya zuio la mumewe akae mbali na mkewe kesi iliyokua imefunguliwa na mkewe kwenye mahakama ya nchi hiyo ya Ubeligiji na muda huo wawili hao walikua kwenye hawaishi pamoja wakati swala lao la talaka likiendelea.

Elizabeth alimwambia mumewe huyo aondoke nyumbani kwake kwani mahakama ilishatoa zuio la yeye kutofika hapo nyumbani lakini James alikataa kuondoka na kuanza kumpiga na kuanza kumchoma visu mara kadhaa na hatimae kumsababishia kifo.

James Ololo baada ya kumuua mkewe aliwaita majirani majirani  wapige simu polisi na yeye alikamatwa na kufunguliwa mashataka ya kuua.

Majirani wamesema James Ololo hua akimpiga mkewe mara kwa mara ugomvi unaosababishwa na yeye anapokua amelewa na zuio la mahakama na kumuzuia yeye asikanyage nyumbani kwake lilimfanya James Ololo kutojimambua na hakua tayari kuachana na mkewe.

No comments:

Post a Comment