Mbowe na Viongozi 8 wa CHADEMA wamemkataa Hakimu

Vigogo tisa wa Chadema akiwemo mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe wamewasilisha ombi la kutaka Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Wilbard Mashauri kujitoa kusikiliza shauri lao.

Kufuatia ombi hilo, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepanga Julai 5, 2018 kutoa uamuzi katika kesi inayowakabili viongozi hao.

Uamuzi huo wa mahakama umetolewa jana Jumatatu Julai 2, 2018 na Mashauri baada ya  washtakiwa hao  kueleza sababu ya kutokuwa na imani nae.

“Baada ya kusikiliza sababu za washtakiwa walizotoa hapa mahakamani za kumtaka hakimu anayeendesha shauri hili kujitoa, Julai 5 mahakama hii itatoa uamuzi kama hakimu huyo ajiondoe kuendesha shauri hilo au asijiondoe” alisema hakimu Mashauri.

Wakili wa utetezi, Peter Kibatala alisema wateja wake wamemueleza kuwa hawana imani na hakimu Mashauri anayeendesha kesi hiyo na wanaomba ujitoe kusikiliza shauri hilo, hivyo wanaomba nafasi ili waweze kueleza sababu za kutokuwa na imani nae.

No comments:

Post a Comment