VIDEO: Ajali yaua watalii wanne Arusha, yajeruhi wawili

Watu Sita wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa kwenye ajali ya barabarani iliyotokea eneo la Nanja Wilayani Monduli Mkoani Arusha baada ya gari la Watalii aina ya Toyota land cruiser kugongana uso kwa uso na gari la mizigo aina ya Semi trela lililokuwa likitokea Mkoani Kigoma kuelekea Nchini Kenya. 

Katika ajali hiyo iliyotokea jana Septemba 02,2018 majira ya saa tatu asubuhi waliopoteza maisha ni Watalii Wanne, Dereva moja na mpishi waliokuwa kwenye gari ya Watalii yenye namba za usajili T 418 AHX mali ya kampuni ya Tabia Safari iliyokuwa ikitokea Mjini Arusha kuelekea hifadhi ya Wanyama ya Tarangire.

No comments:

Post a Comment