Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (katikati) akifurahia jambo na waandishi wa BBC, Salim Kikeke (kulia) na Zuhura Yunus alipotembelea makao makuu ya chombo cha habari cha BBC, mjini London nchini Uingereza kwa ajili ya kufanyiwa mahojiano, juzi. Picha na Mtandao
By Mwandishi Wetu, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz
Dar es Salaam. Majibizano kati ya Tundu Lissu na Spika Job Ndugai yamezidi kukua baada ya mbunge huyo wa Singida Mashariki (Chadema), kuhoji maswali lukuki kuhusu taarifa za matatizo yake akijibu hoja kwamba hana kibali cha kuwa nje ya nchi.
Juzi, Lissu alitoa waraka alioupa jina la “Baada ya Risasi Kushindwa, Sasa Wanataka Kunivua Ubunge”, ukieleza tuhuma zake dhidi ya Serikali kuwa kuna mpango wa kumvua uwakilishi wake wa Singida Mashariki.
Lakini Spika Ndugai aliiambia Mwananchi juzi madai hayo ya Lissu ni “uzushi”, akieleza kuwa Lissu anapaswa kutambua “hana ruhusa ya Spika ya kuwa huko anakozurura”.
“Yeye ametoka kuugua aache uzushi, arudi nyumbani. Tunamsubiri nyumbani,” alisema Spika Ndugai juzi.
No comments:
Post a Comment