LISSU AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA WATANZANIA DMV

Katika mkutano huo Mhe. Tundu Lissu aliyendelea kuyasemea yale alikukua akiendelea kuyasemea alipokua kifanya mahojiano na vituo vya luninga na vyuo katika nchi mbalimbali za Ulaya na Marekani.


Katika mkutano huo Mhe. Lissu ameseama kwamwe hata acha kutetea haki za binadamu na hatasita kukemea unyanyasaji wa dhahili unaofanywa na Serikali ya chama tawala dhidi ya vyama vya upinzani.

Mhe, Tundu Lissu alienda mbali zaidi na kusema kwamba kauli za Mhe Rais ni kuhakikisha kuua nguvu ya upinzani unakufa ifikapo uchaguzi 2020.

Moja ya maswali yaliyoulizwa katika mkutano huo ni kama ana mpango wa kurudi Tanzania, Mhe. Lissu alijibu kwa kusema kurudi Tanzania atarudi lakini yote yanategemea na Daktari wake atakavyomwambia, pamoja na kutolewa ushauri wa wadau kwamba asirudi Tanzania, Mhe. Lissu alisisitiza kurudi Tanzania hakina mjadala. ni lazima arudi kuendeleza mapambano dhidi ya unyanyasaji wa serikali dhidi ya uhuru wa kujieleza na mpango wao wakutokomeza upinzani.

Mhe. Lissu pia aliwaambia waTanzania hao kuhusiana na Bunge kusitisha mshahara wake, aliwaomba waTanzania Diaspora waendelee kumchangia kama walivyofanya kipindi cha matibabu.
Mhe. Tundu Lissu akiongea na waTanzania DMV katika mkutano wake siku ya Jumamosi Feb 9, 2019 mkutano ambao ulijaza ukumbi uliowajumuisha waTanzania wa DMV na wengine waliotokea majimbo mengine.
Mhe. Lissu (kushoto akiongea na waTanzania DMV na majimbo ya jirani waliohudhuria katika mkutano wake uuliofanyia siku ya Jumamosi Feb 9, 2019 Langley Park Maryland. Kulia ni Mwenyekiti wa CHADEMA DMV Kalley  Pndukizi na kati ni mke wa Mhe. Tundu Lissu Bi. Alicia Magabe ambaye pia ni wakili.
Juu na chini ni waTanzania waliohudhuria mkutan wa Mhe.Tundu Liissu


Kwa picha zaidi bofya soma zaidi

No comments:

Post a Comment