Mbeya. Viongozi na wafuasi wa Chadema wamepiga kambi nje ya wodi namba sita Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya alikolazwa Mdude Nyagali maarufu Mdude Chadema tangu alipopatikana usiku wa kuamkia leo Alhamisi Mei 9, 2019 akiwa hai lakini hoi.
Nyagali aliyetekwa na watu wasiojulikana Jumamosi iliyopita akiwa ofisini kwake Vwawa-Mbozi, mkoani Songwe amefikishwa katika hospitali hiyo kwa ajili ya matibabu.
Alifikishwa katika hospitali hiyo jana saa 5 usiku baada ya kuchukuliwa eneo la Inyala, Mbeya vijijiji alikotelekezwa.
Wasamaria wema walimuona akiwa eneo hilo na kumuokota kisha kutoa taarifa kwa viongozi wa Chadema ambao walikwenda kumchukua usiku.
Viongozi walioko hospitalini hapo ni Makamu Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Nyasa, Sadrick Malila, Katibu wa Chadema Kanda hiyo, Emmanuel Masonga na viongozi wengine.
Mbali na viongozi hao, pia maofisa wa vyombo vya ulinzi na usalama wanapishana wodini hapo huku wakiendelea kuchukua taarifa muhimu kutoka kwa Mdude.
No comments:
Post a Comment