Polisi wa kutuliza ghasia, wakifanya doria
kwenye mitaa ya jiji la Mwanza baada ya kutokea ghasia kufuatia askari wa jiji
hilo kufanya jaribio la kuwaondoa wamachinga kwenye soko kuu, rwagasore na mtaa
wa Lumumba mapema leo Jumatano Novemba 19, 2014
Polisi wa kutuliza ghasia wakiwa wamejihami
kwa silaha wakati wakituliza ghasia za wamachinga kwenye mitaa ya jiji hilo
mapema leo Jumatano Novemba 19, 2014. Zogo hilo lilizuka baada ya askari wa jiji
walipowavamia wamachinga na kuwaamuru waondoke kwenye maeneo ya soko kuu,
Rwagasore na mtaa wa Lumumba na hapo ndipo "Kasheshe" lilipozuka ambapo askari
wa jiji walizidiwa nguvu kutokana na mawe yaliyokuwa yakirushwa na wamachinga
mithili ya maroketi na kuwafanya warudi nhyuma na ndipo polisi wa kutuliza
ghasia walipoitwa na kuwakabili wamachinga hao.
Moja ya barabara za jiji la Mwanza ikionekana
kuwa nyeupe huku watu wachache wakitafuta mahala salama baada ya polisi
kupambana na wamachinga mapema leo Jumatano Novemba 19, 2014
Machinga, akirusha jiwe, wakati polisi wa
kutuliza ghasia walipoingia mtaani na kupambana na wafanyabiashara ndogondogo
jijini Mwanza maarufu kama wamachinga, leo Jumatano Novemba 19, 2014




No comments:
Post a Comment