Tatizo la kuvimba miguu kwa wajawazito

Left ankle sprain swelling from trauma on white background.

Akina mama wengi huwa wanapata matatizo ya kuvimba miguu wakati wa ujauzito kwa sababu mbalimbali.
Wengine huwa ni kawaida kwa maana ya kwamba haisababishwi na ugonjwa wa aina yoyote.
Wakati mimba inapokua kubwa huweza tumbo la uzazi Uterus hukandamiza mishipa ya damu inayorudisha damu kwenye moyo Veins au ile mishipa inayobeba maji damu lymph kutoka kwenye miguu.
Hali hiyo hufanya damu na hayo maji damu kushindwa kurudi yote kwenye moyo na kujikusanya sehemu ambazo ni Dependent hasa miguuni na kusababisha uvimbaji wa miguu Dependent Oedema.
Uvimbaji huu ni ule ambao sana uko kwenye sehemu ya mguu chini ya kifundo cha mguu Ankle Oedema, kama miguu ikivimba kupanda juu hadi kwenye mapaja au juu zaidi hii huwa ni dalili ya ugonjwa.
Magonjwa ambayo yanaweza kusababisha uvimbe miguuni na sehemu nyingine za mwili wa mjamzito ni pamoja na kuwa na shinikizo la damu la ujauzito Pre-eclampsia, magonjwa ya figo ambapo mtu huvimba miguu, uso pia, magojwa ya ini – haya husababisha pia maji kujaa kwenye ukuta wa mbele wa tumbo Ascites lakini pia mwili wote waweza kuvimba.
 Mtu anaweza kuvimba miguu kutokana na kuwa na ukosefu wa protini kwenye damu Hypoproteinaemia kwa sababu yoyote, ugonjwa wa moyo Heart Failure n.k.
TIBA NA USHAURI
Ni vizuri mjamzito anapovimba miguu aende hospitali kwa ajili ya uchunguzi, atatibiwa kulingana na tatizo litakalogundulika.
Kama ni ile Dependent Edema, anachotakiwa ni kutosimama kwa muda mrefu na hata akikaa miguu asiining’inize, pia wakati wa kulala asipende kulalia mgongo yaani kichalichali kwani hii husababisha mfuko wa uzazi Uterus kukandamiza hiyo mishipa ya damu na kusababisha uvimbe miguuni kama nilivyoeleza juu.

No comments:

Post a Comment