Mtoto Latifa aliyeibiwa asubuhi saa 2 Iringa Mjini apatikana usiku kijiji cha Mkungugu

Leo mida ya saa 2 asubuhi katika maeneo ya Stand kuu ya mabasi aliibiwa mtoto mchanga mweney umri wa miezi 5. Mtoto huyo aliibiwa na binti ambaye alikuwa amekuja kutafuta kazi. Akieleza tukio hilo Mama yake Bi Asha Shaban Lauza alisema " nikiwa naosha vyombo binti huyu ambaye toka jana alikuwa anatafuta kazi alianza kumpa maziwa mtoto yaliyo kwenye chupa mpaka mtoto akamaliza , baadae mtoto akajinyea basi bila wasiwasi nikampa shilingi elfu kumi ili akanunue pampasi duka la pili tu akanyanyuka na mtoto kwenda dukani toak asubuhi mpaka sasa usiku hautja muona" .

 Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela alifika eneo la tukio baada ya kumhoji mzazi akagundua walichelewa kutoa taarifa polisi. Baada ya msako muda was saa 3 usiku mtoto alipatikana eneo la Mkungugu km 33 kutoka Iringa Mjini. Binti wa miaka 14 (Jina linahifadhiwa) alikuwa akitoroka na mtot huyo gari la polisi la doria likishirikiana na wananchi wa kijiji cha Mkungugu lilifanikiwa kumuweka chini ya ulinzi mwizi huyo wa mtoto. 

Mkuu wa Wilaya alifika akiongozana na mama Mzazi wa mtoto pamoja na Diwani wa kata ya Kisinga Mh Ritha Mlagala. Binti mwizi yupo kituo cha polisi akiendelea kuhojiwa na mama mzazi baada ya kuandika maelezo alipewa fomu ya matibabu na kumpeleka mtoto hospitali. Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela amekemea vikali kitendo cha uzembe wa mama huyu na wazazi kwa ujumla "pamoja na mama huyu kuwa na uchungu wa mtoto bado ana mashtaka ya kujibu ya uzembe, watu tusio wajua tusiwape watoto wetu hata kidogo huu ni uzembe wa hali ya juu" alisisitiza Mkuu wa wilaya. Pichani anaonekana mtoto Latifa akiwa ambebwa na Mkuu wa wilaya walipofika kituo cha polisi. Picha zingine ni za eneo la kijiji cha Mkungugu barabani alipokamatwa binti mwizi akiwa na mtoto usiku wa saa 3.​

Waziri Nape: Sikupinga vita dhidi ya biashara ya dawa za kulevya bali nilishauri busara itumike

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ametoa ufafanuzi juu ya kauli iliyonukuliwa ikionyesha kuwa alipinga vita dhidi ya dawa za kulevya iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Amedai kuwa hakupinga vita hiyo bali alitaka busara itumike kwa washukiwa.

Waziri Nape alitoa ufafanuzi huo katika kipindi cha dakika 45 cha ITV, alipoulizwa swali na mtangazaji wa kipindi hicho kutaka kujua kuhusu kauli yake iliyoonesha kupinga utaratibu uliotumika wa kuwakamata au kuwapata watuhumiwa wa dawa za kulevya.

“Niseme kwanza ilitokea nilikuwa na mkutano na waandishi wa habari, ukienda leo ukanitaja Nape ukaniambia baada ya siku mbili njoo kituoni, hata kama nilikuwa na madawa ya kulevya nyumbani kwangu hivi unayakutaje? 

Bush Rebukes Trump on Media, Immigration

In a rare interview, former President George W. Bush rebuked President Donald Trump on his views about the media and immigration.
Speaking with Matt Lauer on NBC’s TODAY show, Bush said the news media are “indispensable to democracy” and said he is in favor of an immigration policy that is “welcoming and upholds the law.”
Trump has called the press “fake” and “the enemy of the people,” a view Bush does not share. Bush told Lauer that he often tried to convince leaders like Russian President Vladimir Putin to “accept the notion of an independent press,” adding, “and it’s kind of hard to, you know, tell others to have an independent, free press when we’re not willing to have one ourselves.”
- The Daily Beast

Lori laporomoka mlimani, laua wafanyabiashara 6 na Kujeruhi 12

Wafanyabiashara sita wamekufa papo hapo na wengine 12 kujeruhiwa, baada ya lori lililokuwa likiwapeleka mnadani kuacha njia na kuporomoka kwenye mlima wenye kona nyingi zinazofikia 99 wilayani Lushoto.  Taarifa zilizopatikana na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba zilisema ajali hiyo ilitokea jana Jumapili jioni katika mlima wenye idadi hizo za kona...
Read More

AUDIO: Askofu Gwajima aelezea sakata zima la Makonda kutumia vyeti vya mtu mwingine

Siku kadhaa baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kusema kuwa hawezi kujibu madai ya mitandao ya kijamii kuwa alitumia vyeti vya mtu cha kidato cha nne, Askofu Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima ameibuka na kusema kuwa ni kweli alitumia vyeti hivyo. Askofu Gwajima amesema kuwa anamfahamu sana Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na kuwa jina lake halisi ni Daudi Bashite na kwamba...
Read More

Mahakama yaicharukia serikali kesi ya Godbless Lema......Yahoji sababu za mbuge huyo kunyimwa dhamana.

Mwenyekiti wa kikao cha jopo la Majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa, kinachoendelea Arusha, Bernard Luanda, leo amegeuka mbogo kwa wanasheria wa serikali kwa kitendo cha kumnyima Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema dhamana kwa lengo la kumnyima haki. Akizungumza Mahakamani hapo leo mbele ya majaji wenzake Stella Mugasha na Jaji Kipenka Mussa, Luanda amesema haipendezi na haingii akilini mtu...
Read More

CHADEMA Wamwandalia Sherehe Wema Sepetu

Chama cha Demokrasi na Maendeleo (Chadema), kimesema kipo kwenye maandalizi ya kumkabidhi kadi mrembo wa Tanzania mwaka 2006, Wema sepetu, pamoja na kundi lake lenye zaidi ya watu 500.

Wema alikuwa mmoja kati ya wanachama maarufu wa CCM katika kundi la wasanii wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka juzi kwa kaulimbiu ya ‘mama ongea na mwanao’.

Akiwa kama kiongozi wa wasanii, alishiriki kumnadi Mgombea Mwenza wa CCM ambaye kwa sasa ni Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan.

Katika mkutano wake na wanahabari mwishoni mwa wiki,  Wema  alisema kwa sasa ameamua kuvaa magwanda na yupo tayari kwa mapambano.

Mkuu wa Idara ya Habari wa Chama cha Demokrasi na Maendeleo (Chadema), Tumaini Makene jana alisema   wapo kwenye maandalizi na kabla ya Machi 5, mwaka huu watamkabidhi Wema kadi ya uanachama   na kundi lake linalomuunga mkono.

SAMANI ZA NDANI ZAMNG’ARISHA JACQUELINE NTUYABALIWE KWENYE FORBES

KATIKATI ya foleni katika jiji la Dar es Salaam ndani ya gari nyeupe aina ya Mercedes S550, Jacqueline Ntuyabaliwe, mrembo wa miaka 38, macho yake yalikuwa yametulia katika simu yake ya mkononi. Alikuwa akiangalia seti ya samani za eneo la kulia chakula. Kwa bashasha, baada ya muda kidogo anatanua picha hiyo kisha ananisogezea simu yake ya mkononi kunionesha picha anayoiangalia. “Hii ni moja ya samani tulizonazo,” anasema huku akinionesha seti hiyo ambayo imetengenezwa na Molocaho by Amorette, kampuni ya kutengeneza samani aliyoianzisha hivi karibuni. “Samani hizi zimetengenezwa kutokana na mbao zilizotwaliwa kutoka katika mashua za zamani za mizigo kwenye fukwe za Tanzania upande wa bahari ya Hindi,” anasema mjasiriamali huyo. Samani hizo za eneo la kulia chakula (Dining Table) anasema zimeagizwa na familia moja iliyopo Ulaya ambayo siku za karibuni ilitembelea duka lake (showroom) Dar es Salaam wakati wakiwa likizo na kwamba anajiandaa sasa kuisafirisha seti hiyo ya samani kwa wateja wake wapya wa Ulaya. Lakini kwanza alichokuwa anakifanya kwa siku ile ni kwenda kiwandani kuangalia seti hiyo ya samani kwa mara ya mwisho kabla ya kusafirishwa ili kujihakikishia kwamba imemaliziwa urembeshaji kwa namna inavyotakiwa kuwa.
Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi.

Jacqueline Ntuyabaliwe, anayetaka umaridadi uliokamilika, ni binti ambaye huangalia vitu vidogo vidogo kuona kama vipo sawa katika hali inayokubalika viwe. Pamoja na kuwa na ratiba yenye changamoto sana (Yeye ni Balozi wa WildAid na yumo ndani ya bodi kadhaa; mama wa watoto pacha wavulana; mke kwa mfanyabiashara mwenye mafanikio makubwa na akiendesha taasisi ya hisani ya elimu), Ntuyabaliwe huhakikisha anakagua kila samani inayozalishwa kiwandani kwake kabla ya kuuzwa au kusafirishwa. “Napenda kitu bora chenye uhakika!” anasema mlimbwende huyo wa zamani wa Tanzania ambaye pia ni mwanamuziki. “Kila kitu tunachokifanya Molocaho lazima kiwe chenye uhakika hakina makosa wala dhaifu, lazima kiwe kimetulia,” anasema mrembo huyo. “Tunashindana na watu maarufu duniani wanaofanya vyema kwa hiyo kama sisi tusipofanya vyema kuliko wao tutashindwa,” aliongeza. 

Ntuyabaliwe, mzaliwa wa Tanzania, aliyefunzwa kubuni uzuri wa ndani, ni mwanzilishi na mbunifu mkuu wa Molocaho by Amorette, kampuni ya Tanzania inayojishughulisha na utengenezaji wa samani bora kwa namna mteja anavyohitaji, samani, nyuzi, taa, urembaji, samani za nje na kwenye bustani. Molocaho inatengeneza samani zenye mahadhi ya kiafrika ikichanganya utamaduni wa Tanzania katika mazingira ya kisasa na kumalizia na ubunifu wa kimataifa. Molocaho, moja ya makampuni ya Afrika Mashariki ya samani yanayokua kwa kasi, imejipatia nafasi kubwa ya heshima kwa kuhakikisha kwamba inatumia mali ghafi na mbao njema pekee za Tanzania kutengeneza samani zenye kwenda kimataifa. “Mpango wetu mkubwa ni kujenga nembo ya biashara ya samani za Tanzania inayotambulika kimataifa. Ni dhahiri itatuchukua muda kufikia huko , lakini 

MBIO ZA TIGO KILI HALF MARATHON ZAFANA MJINI MOSHI


Sehemu ya kuanzia ya Tigo half Kilimarathon yaliyofanyika Moshi, Kilimanjaro.
Washiriki wa Tigo half Kilimarathon wakiwania taji hilo kwenye mashindano hayo yaliyofanyika Moshi, Kilimanjaro

Kichupa cha leo young killer MSODOKI - Sinaga swagga (official Video)

Wizara ya Mambo ya Nje yahamishia Ofisi zake Dodoma Rasmi

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Ofisini kwake Mjini Dodoma. Waziri Mahiga leo ameutangazi Umma wa Watanzania kuwa Wizara imehamia rasmi Dodoma. 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KUHUSU WIZARA KUHAMIA DODOMA
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inapenda kuufahamisha Umma kuwa tayari imeshahamia Dodoma kuanzia tarehe 17 Februari, 2017.  Hatua hiyo imehusisha Awamu Mbili, Awamu ya kwanza imetekelezwa tarehe 28 Januari, 2017 na Awamu ya Pili imetekelezwa tarehe 17 Februari, 2017.
Miongoni mwa Watumishi waliohamia Dodoma katika awamu hii ya kwanza (Awamu ndogo ya kwanza tarehe 28 Januari, 2017) nipamoja na Viongozi Wakuu na Watumishi wa Wizara wakiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.  Dkt. Augustine P.Mahiga na Naibu Waziri Mhe. Dkt. Susan A. Kolimba pamoja na Watumishi Kumi (10) waliofuatana nao. Awamu ndogo ya kwanza ilifuatiwa na (Awamu ndogo ya Pili tarehe, 17 Februari, 2017) iliyoongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara, Balozi Dkt. Aziz P.Mlima na Naibu Katibu Mkuu Balozi Ramadhan M.Mwinyi wa kiongozana na Watumishi 33 wa Wizara ya Mambo ya Njena Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Kenya receives Washington’s approval for direct US flights


JKIA
PHOTO:Terminal 1A at the Jomo Kenyatta International Airport in Nairobi. PHOTO | FILE /NATION
 
ShareThis
Share

By:
GERALD ANDAE 
Posted:
Feb,24-2017 17:08:37
 
Inspectors from America's FAA gave Jomo Kenyatta International Airport a clean bill of health after an audit leading to the award of the long awaited Category One status.
This sets the stage for signing of flight agreements between Washington and Nairobi as well as airlines seeking direct flights between the US and Kenya before commercial operations can start.
Kenya, which hosted President Barack Obama in July 2015, wants to boost exports to Washington and increase visits by American tourists. Starting flights was part of a package of deals announced during Obama's visit. "Kenya has today been granted Category One status by the US Government following a meticulous assessment audit by the FAA and other US agencies," said a statement from the Transport ministry.
"The granting of this status means that airline operators, both in Kenya and the US, which have long desired to operate directly... will now be allowed to carry on their operations after certain processes including technical compliance and commercial arrangements are met."
The FAA was meant to issue a statement by time of going to Press yesterday. The second class status of JKIA means passengers flying from Kenya to the US have to transit through Europe, the Middle East or any of the four African countries whose airports have achieved the Category One status. These are South Africa, Ethiopia, Cape Verde, and Nigeria.
Delta Airlines previously set a launch date for direct flights but cancelled due to security concerns.
Financially embattled Kenya Airways also plans to offer direct flights. US traffic usually transits through hubs like Dubai and Amsterdam. JKIA failed the US safety review in 2013 but has since improved security through upgrades.
New terminals have been opened over the past three years, allowing the airport to separate departures and arrivals, a key security requirement.
"With Category One there will be faster movement of goods and people between the two countries, with an eradication of any delay especially to horticultural produce from Kenya," the statement said.
In order to attain and maintain the rating, a country must demonstrate compliance with safety standards contained in the International Civil Aviation Organisation's practices for aircraft operations and maintenance.
Kenya has been implementing a raft of recommendations by the US government to enhance security, among them separation of passenger arrival and departure terminals, clearing the flight path and fencing off the airport.

I Cut My Husband's Manhood, Kenyan Woman Tells Court

I Cut My Husband's Manhood, Kenyan Woman Tells Court

A woman on Monday admitted in a Mombasa court that she cut her husband’s manhood.
Angel Mutuku pleaded guilty to a charge of causing actual bodily harm to Stephen Ochieng Oyuga.
The prosecution said Mutuku unlawfully assaulted Mr Oyuga in Changamwe, Mombasa County, on February 16.
Prosecutor Lydia Kagori told Chief Magistrate Julius Nagea to defer the case until Wednesday, when the facts of the case will be read to the accused.
“We wish to present the facts of the case on Wednesday. There may be more charges preferred against the accused person as the state of the complaint is not good,” added Ms Kagori.
Mr Oyuga is being treated at Bomu Medical Centre.
The woman is said to have grabbed a kitchen knife and cut her husband’s manhood after a quarrel.
The woman, in her statement to the police, said she woke up her husband but he was offended and a quarrel ensued.
Ms Mutuku was pushed to the ground but she rose and went to the kitchen, where she took a knife, grabbed the husband’s manhood and cut it.
She is said to have gone to work, leaving the man writhing in pain but called his brother to take him to hospital.
- Nation.co.ke

Picha 8 za Mbowe, Lowassa , Nape na Wema Sepetu Walivyoshuhudia Yanga Ikitandikwa Mabao Mawili na Simba

Baadhi ya Viongozi wa Serikali na Siasa leo walikuwa miongoni mwa watu walioshuhudia mpambano kati ya watani wa jadi Simba na Yanga katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, ambapo mnyama Simba ameibuka kidedea kwa kuibamiza Yanga goli 2-1 licha ya kuwa pungufu kwa muda mref...
Read More

Kikwete: Siasa ni shule isiyokuwa na mwisho

Mbunge wa Chalinze mkoani Pwani kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Ridhiwan Kikwete, amesema siasa ni shule ambayo haina mwisho na ndiyo maana anaendelea kujifunza mengi kutoka kwa wanasiasa wenzake husani waliomtangulia bila kujali chama. Kikwete alitoa ujumbe huo jana  mara baada ya kukutana na kuteta na aliyekuwa mgombea urais kupitia CHADEMA katika uchaguzi wa mwaka 2015, Edward Lowassa...
Read More

Magufuli, Museveni wagomea EPA

RAIS John Magufuli na mgeni wake Rais wa Uganda, Yoweri Museveni wamekubaliana kuhakikisha wanatumia fursa zilizopo kuongeza biashara kati ya nchi hizo ili kukuza uchumi wa nchi hizo mbili. Rais Museveni yupo nchini kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili, ambapo jana alikuwa na mazungumzo ya kina na Rais Magufuli.
Akizungumza na waandishi wa habari, Rais Magufuli alibainisha kuwa mazungumzo yao pia yalilenga suala la kusaini Mkataba wa Ushirikiano wa Kibiashara (EPA) na nchi za Jumuia ya Ulaya (EU).
Rais Magufuli alisisitiza kuwa Tanzania haitasaini mkataba wa EPA na kubainisha kuwa hiyo ni njia nyingine ya ukoloni.
“Tumezungumza kwa kina na Rais Museveni na tumekubaliana kuendelea kulizungumza. Nimemueleza kuwa sisi Tanzania tunaona EPA haina faida na ni ukoloni mwingine, ambao unaletwa kwa sababu ya mambo mengi.
“Hatuwezi kuzungumzia kujenga viwanda wakati huohuo tunashindana na watu wenye viwanda vikubwa.
“Hili tumelizungumza kwa kina na tumekubaliana na Rais Museveni na jopo la wataalamu litakwenda Uganda Machi 18, kutoa maelezo ya kina. Na yeye Rais Museveni amesema kimsingi anapenda kufanya kitu chenye faida.” Rais Magufuli aliongeza:

VIGOGO 4 WA SHIRIKA LA POSTA WATUMBULIWA

BODI ya Wakurugenzi wa Shirika la Posta Tanzania, imetengua nafasi tatu za mameneja na ofisa mwandamizi kutokana na vitendo vya umangimeza, urasimu, kufanya kazi kwa mazoea, ubadhirifu na wizi.

Mameneja waliotenguliwa ni James Sando ambaye alikuwa Meneja Mkuu, Menejimenti ya Rasilimali. Macrice Mbodo ameteuliwa kushika nafasi hiyo.

Mwingine aliyetenguliwa ni Meneja Mkuu Uendeshaji wa Biashara Janeth Msofe. Aliyekuwa Meneja wa Mkoa Shinyanga, Hassan Mwang'ombe kateuliwa kushika nafasi hiyo.

Bodi pia imewasimamisha kazi Meneja Msaidizi wa Barua na Logistic, Jasson Kalile na Ofisa Mwandamizi wa Usafirishaji, Ambrose John.

The God Who Goes Before You - Joel Osteen


Rais Magufuli awapongeza madaktari Muhimbili na amsaidia Neema Mwita Wambura aliyeunguzwa moto kifuani

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewapongeza Madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa juhudi kubwa walizofanya kunusuru maisha ya Neema Mwita Wambura ambaye alijeruhiwa kwa kuunguzwa na maji ya moto kifuani, shingoni na mkononi. Pongezi hizo za Mhe. Dkt. Magufuli zimetolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Bw. Gerson Msigwa muda mfupi...
Read More

Taarifa Kuhusu UTAPELI Ajira za JWTZ


Makonda agoma kuzungumzia kughushi vyeti



Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda
By Elizabeth Edward, Mwananchi

Dar es Salaam. Licha ya kuandamwa na tuhuma za kughushi vyeti, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema hawezi kuzungumzia suala hilo kwani majibu yake yapo mtandaoni sakata lilipoanzia.

Makonda amesema hayo leo (Ijumaa) alipoulizwa swali na wanahabari kuhusu uhakika wa taarifa zinazosambaa mitandaoni kuwa alinunua vyeti na kutumia jina lisilo lake.

"Maswali ya mitandaoni yanaishia mitandaoni siko hapa kupoteza focus (mwelekeo).Ukiona maneno mengi yanaibuka kwenye ishu ya dawa za kulevya ndiyo ujue vita imefika penyewe,"amesema Makonda.

MSHUKIWA MKUU WA MADAWA YA KULEVYA AKAMATWA-BBC

Paul Makonda kamishna wa eneo la Dar es Salaam
Maafisa wa polisi nchini Tanzania wanasema kuwa wamemkamata kiongozi wa ulanguzi wa dawa ya kulevya aina ya heroine anayefanya operesheni zake kati ya Afrika mashariki na China.

Maafisa hao wanaokabiliana na ulanguzi wa mihadarati wanasema kuwa Ayub Mfaume ambaye anajulikana kama kiboko alikuwa mmoja wa watu wanaotafutwa sana nchini humo.

Anadaiwa kuwa na ushiirikiano na walanguzi wa mihadarati nchini Brazil, Pakistan, na mataifa kadhaa ya Ulaya.

Maafisa hao wanasema kuwa Bwana Mfaume alijisalimisha kwa maafisa hao kufuatia msako wa wiki mbili dhidi ya walanguzi wa mihadarati

Wema Sepetu akizungumzia sababu za kuihama CCM na kujiunga CHADEMA

Mwanafunzi akipata mimba mzazi jela miaka 30


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amesema serikali itatoa adhabu kali ya kifungo cha miaka 30 jela kwa wazazi wote wawili wa mtoto wa kike atakayekatishwa masomo na kulazimishwa kuolewa ama akipata ujauzito. Aidha amesema Serikali itamfunga jela miaka 30 kijana anayetaka kumuoa msichana anayesoma pamoja na wazazi wake. Amesema Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kumlinda mtoto wa kike katika...
Read More

Wema Sepetu ahamia Chadema, aungana na Mbowe mahakamani

Chama cha Demokrasia na Maendeleo kunatarajia kuwakaribisha wanachama wapya waliojiunga leo na chama hicho akiwamo msanii maarufu nchini wa fani ya uigizaji wa filamu, Wema Sepetu (28...
Read More

Kutoka Mahakamani: Mbowe Kuendelea Kutokamatwa na Polisi Wala Kuwekwa Kizuizini

Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Tundu Lissu ameongea na waandishi wa habari jioni hii  baada ya kutoka Mahakamani  kwenye kesi iliyofunguliwa na Freeman Mbowe dhidi ya Mkuu wa Mkoa w Dar Paul Makonda  na Kamshna Sirro. Lissu amesema Amri ya kuzuia Freeman Mbowe asikamatwe na wala kuwekwa kizuizini na Polisi inaendelea isipokua wanaweza kumuita kwa Mahojiano...
Read More

MKE WA BILIONEA MSUYA AACHIWA HURU

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru mke wa marehemu bilionea Erasto Msuya, Miriam Mrita na mwenzake Revocatus Muyela wanaokabiliwa na kesi ya mauaji ya Aneth Msuya.
Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa leo (Alhamisi) amewaachia huru washtakiwa hao baada ya upande wa mashtaka kushindwa kufanya marekebisho ya hati ya mashtaka ya mauaji ya kukusudia iliyokuwa ikiwakabili mahakamani hapo.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya jalada la kesi hiyo lililokuwa limeitwa Mahakama Kuu kurejeshwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo Februari 20, 2017 Hakimu Mwambapa aliupa upande wa mashtaka muda wa siku tatu kurekebisha hati ya mashtaka.

WOLPER AMTEMA RASMI HORMONIZE

Na WAANDISHI WETU| GAZETI LA AMANI| HABARI NA GPL

DAR ES SALAAM: Msanii wa sinema za Bongo, Jacqueline Wolper amefunguka kuhusu kuachana rasmi na mpenzi wake ambaye ni msanii wa muziki kutoka Kundi la Wasafi Classic Baby ‘WCB’, Rajabu Ibrahim ‘Harmonize’.

Akizungumza na mwandishi wetu jana, Wolper alikiri kwamba, yeye na Harmonize, mapenzi yao yamekwisha kabisa.

“Yah! Ni kweli, nimeamua tu kuachana naye. Unajua katika uhusiano kuna kugombana, tumekoseana na kusameheana mara nyingi, sasa tumeamua kila mtu aendelee na maisha yake. Kwangu ni fursa nzuri kwani nitakuwa na amani ya moyo. Maisha yatasonga na nitajikipu ‘bize’ na kazi zangu. “Siwezi kujutia uamuzi huu na moyo wangu umeshazoea, kanikuta nikiwa Wolper na tumeachana nikiwa Wolper labda kama angekuwa amenikuta Fatuma na kunifanya kuwa Wolper.

“Harmonize nimedumu naye kwenye mapenzi kwa mwaka mmoja tu. Nilimkosea, akanikosea kanikosea tena, siwezi kuongelea kitu halisi alichonikosea lakini jua hilo.

“Wakati tukiwa kwenye uhusiano wetu hatujawahi kuchiti (kusaliti) au inawezekana tulichiti na tukasameheana ila kwangu ni rahisi kusamehe kwa kuchiti kuliko kukusamehe kwenye kosa dogo ambalo wewe unaliona ni la kawaida lakini kwangu nikahisi kama unanishusha thamani, na ninapoingia kwenye uhusiano huwa nasema vitu ambavyo sivipendi kukosewa, na nikiona unakosea mara kwa mara najua hiyo ndiyo tabia yako,” alisema Wolper na kuongeza:

“Hata sikumbuki mara ya mwisho niliongea naye lini ila neno lake la mwisho kwangu lilikuwa ni samahani ambalo sijalikubali.” Juhudi za kumpata Harmonize zinaendelea baada ya jana kutokupatikana hewani.

WAFANAYAKAZI 14 WA MANJI WAFIKISHWA MAHAKAMANI

Raia 14 wa India ambao wanafanya kazi Quality Group iliyo chini ya Yusuf Manji leo wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka matatu likiwemo la kufanya kazi nchini bila ya kuwa na kibali.

Washtakiwa hao wamesomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha.

Hati ya mashtaka, iliyosomwa na mwendesha Mashtaka, wa uhamiaji Method Kagoma imewataja washtakiwa hao kuwa ni Rojat Surkar, Jagadish Mamidu, Niladri Maiti, Sivarar Raja Sekaran, Mohammed Taher Shaikh, Bijenda Kumar, Prasoon Kumar Mallik na Nipun Dinbandhu Bhatt.

Wengine ni Pintu Kumar, Anuj Agurwa, Varun Boloor, Arun Kumar Kateel, Avinash Chandratiwari na Vikram Sankhala.

Akisoma hati ya mashtaka, Kagoma amedai kuwa, Februari 13, mwaka huu, huko katika ofisi ya Quality Group Ltd iliyopo katika Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, washtakiwa hao walikutwa wakiwa na viza zilozoghushiwa za kufanyia kazi.

RAIS DKT. MAGUFULI AMSAIDIA DADA NEEMA MWITA WAMBURA ALIYEMWAGIWA UJI WA MOTO NA MUMEWE MKOANI MARA.

 Dada Neema Mwita Wambura (32) akizungunza na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kupitia njia ya Simu akimshukuru kwa msaada aliompatia wa kufanyiwa tena uchunguzi wa afya yake katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Pia Rais Dkt. Magufuli ameahidi kumpatia hifadhi mama huyo pamoja na watoto wake watatu ambao kwa sasa wapo Bunda mkoani Mara. Pia Rais Dkt. Magufuli alimpatia msaada Dada huyo kiasi cha Shilingi laki tano.  Dada Neema Mwita Wambura aliungua vibaya mara baada ya kumwagiwa uji wa moto uliokuwa unachemka jikoni na mume wake katika kijiji cha Kyagata, Tarime mkoani Mara.
 Mama Mjane Mariam Amir ( Bibi Mwaija ) ambaye amempa hifadhi Neema Mwita Wambura nyumbani kwake Tandika Davis Corner akiomba dua kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kupitia njia ya Simu kumshukuru mara baada ya kuzungumza naye kuhusiana na kumsaidia Dada Neema Mwita Wambura (32). Rais Dkt. Magufuli amempongeza Mama huyo Mjane ambaye ameonesha moyo wa kizalendo na kumpa hifadhi Dada huyo aliyemwagiwa uji wa moto na mumewe katika kijiji cha Kyagata, Tarime mkoani Mara. Pia Rais Dkt. Magufuli alimpa Mjane huyo kiasi cha Shilingi laki tano.

WENGI WAJITOKEZA KUMUAGA MWANA TBN JENNIFER LIVIGHA (CHINGA ONE) HOSPITALI YA AMANA JIJINI DAR

Pichani Mpendwa wetu Jennifer Livigha aliyekuwa Mmiliki wa Libeneke la Chinga One na Mwanachama wa TBN Enzi za uhai wake. Marehemu alizaliwa 25.01.1979 Nachingwea, alifariki nyumbani kwake kinyerezi 18.02.2017 Jijini Dar es salaam. Marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa Ini. Atapumzishwa katika nyumba yake ya milele nyumbani kwao Nachingwea.
 Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika Ibada ya kuaga Mwili wa Marehemu Jennifer Livigha aliyekuwa mmiriki wa Blog ya Chinga One katika Hospitali ya Amana.
 Waongozaji wa Ibada ya kuaga mwili wa Marehemu Jennifer