Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Umeme Vijijini
(REA), Lutengano Mwakahesya (PhD) (kushoto), pamoja na Mkurugenzi Mwendeshaji wa
Kampuni ya Off Grid Electric Ltd, wakionesha seti ya mfumo wa vifaa vya umeme wa
sola ambavyo vitatumika katika mpango wa kutumia umeme wa sola kwa nyumba
milioni 1 wakati wakiwaonesha waandishi wa habari Dar es Salaam leo
asubuhi.
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Umeme Vijijini
(REA), Lutengano Mwakahesya (PhD) (kulia), pamoja na Mkurugenzi Mwendeshaji wa
Kampuni ya Off Grid Electric Ltd, Erica Mackey wakiteta jambo wakati wa mkutan
huo na waandishi wa habari.
Meneja wa Miradi Maalumu wa Kampuni hiyo,
James Sawabini (kulia), akiandaa vifaa hivyo kabla wakati vikioneshwa kwa
waandishi wa habari.
Wapiga picha kutoka vyombo mbalimbali vya
habari wakichukua taarifa hiyo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
SERIKALI ya Tanzania imesema hadi ifikapo mwaka 2017, itakuwa imetimiza mpango mahususi wa kutumia umeme wa sola uitwao 'One Solar Homes' katika nyumba milioni moja.
Akizungumza Dar es Salaam leo mchana , Mkurugenzi Mkuu wakala wa Nishati Vijijini, Lutengano Mwakahesya, alisema mradi huo unatarajia kutoa huduma ya umeme kwa asilimia 10 ya watu nchini na ajira 15000 zitakazohusu sola.
No comments:
Post a Comment