Update: Kama Bado Hujayaona Matokeo ya Kidato cha Nne.....Yaangalie Kupitia Hapa

Tovuti ya Necta imeelemewa Kidogo. Tumia Hii Link kuyatazama Matokeo ==> Bofya << HAPA>>  Kuyatazama Matok...
Read More

MSIBA WASHINGTON.DC NA TANZANIA



Aunty Martha Marealle wa DMV anasikitika kuwatangazia kifo cha mwanae *Eva Marealle Mwingizi* kilicho tokea Jana 1/29/17 Dar Es salaam,hospital ya TMJ mikocheni.

Address ya Msiba DMV
19 Gallatin st NE
Washington,D.C. 20011

Kwa rambi rambi
Capital One Bank
Name: Martha Marealle
Account# 0113491743
Routing # 255071981

Cashme account: $MarthaMarealle

Contact people;
Britta Mawalla 301 237 3399
Sarah Towo 248 514 0556
Lilu Marealle 703 725 7505
Fofo Madete 202 569 2777

Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe milele.

New Song: Willi Willi Dance - by Kenwizz (3 piece)

Mwili wa Marehemu Saleh wazikwa Philadelphia, Tunawashukuru wote kwa michango yenu


Marehemu Saleh enzi za uhai wake
  Kwa Niaba ya Wanafamilia ningependa kutoa shukran kwa watu wote walioshiriki mazishi ya Marehemu Saleh huko Philadelphia leo, Kwa kweli Mapenzi ya Utanzania wetu bila kujali dini au kabila Watanzania wamejitokeza kutoka Boston, NewYork Connecticut,  Delaware, Georgia, Ohio, Texas na DMV  wapo walio drive masafa marefu na wengine kutumia usafiri wa ndege na wengine kuchangia michango ya online ya Mazishi Tunasema shukran .kwa  upendo huu,
 Marehemu Saleh akiombewa dua baada ya mazishi
 Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki waliofika kwenye mazishi ya Marehemu Saleh

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MARAIS MBALIMBALI WA AFRIKA KATIKA MAKAO MAKUU YA UMOJA WA AFRIKA (AU) MJINI ADDIS ABABA ETHIOPIA


 Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika moja ya Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa kwa ajili ya mazungumzo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma mara baada ya kuwasili kwa ajili ya mazungumzo katika Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma mara baada ya kumaliza mazungumzo yao katika moja ya katika Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.

Kichupa cha leo Nedy Music ft Christian Bella - Rudi ( Official Music Video )


KAMISHNA WA OPERESHENI NA MAFUNZO WA JESHI LA PILISI,NSATO MARIJANI AWAFARIJI ASKARI WALIOPOTEZA MALI ZAO KWA TUKIO LA MOTO MJINI MOSHI.


Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi, Nsato Marijani akiwasili katika eneo lilipo jengo la ghorofa ambalo ni makazi ya sakari lililoungua moto huku akiaongozana na Mwenyeji wake Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Wilbroad Mutafungwa.
Jengo la ghorof mbili ,makazi ya askari Polisi wa vikosi mbalimbali mjii Moshi liliungua moto sehemu ya juu na kueteketeza vyumba tisa pamoja na mali za asakri waliokuwa wakiishi katika vyumba hivyo.

Wachimbaji 15 waliokuwa wamefukiwa na kifusi waokolewa wakiwa hai


Watu 15 waliokuwa wamefukiwa na kifusi Geita waokolewa wakiwa hai. Kwa mujibu wa habari watu hao wamepelekwa hospitali ili kupatiwa matibabu zaidi. Ikumbukwe kuwa watu hao walifukiwa na kifusi hicho wakati wakiwa kazini katika moja ya migodi iliyoko chini ya wachina.

BREAKING NEWS:TRENI YA ABIRIA DELUX YAPATA AJALI IKITOKEA KIGOMA KUJA DAR ES SALAAM


NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
TRENI ya mwendo haraka, (DELUX), iliyokuwa ikitokea Kigoma kuja jijini Dar es Salaam, imeanguka eneo la Ruvu mkoani Pwani jioni hii ya Januari 29, 2017.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka eneo la ajali,zinasema takriban mabehewa 10 yameanguka na juhudi za kuwaokoa watu zilikuwa zikiendelea na watu kadhaa walionekana wakiwa wamelala chini wengine hawajiwezi kabisa.
Msemaji wa TRL, Medladjy Maez amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, na alipoongea na mwandishi wa habari hizi majira ya saa 11;13 jioni, amesema treni hiyo imeanguka na ni mabehewa matano ya abiria yameanguka na moja limeacha njia, lakini hakuwa na taarifa zaidi kwani ndio alikuwa anajiandaa kuelekea eneo la tukio.

RAIS DKT. MAGUFULI AHUTUBIA KATIKA KUTANGAZA JINA RASMI LA KITUO CHA AMANI NA USALAMA KILICHOPEWA JINA LA MWALIMU JULIUS NYERERE KATIKA MAKAO MAKUU YA UMOJA WA AFRICA (AU) ADDIS ABABA NCHINI ETHIOPIA


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia Viongozi Wakuu wa Mataifa mbalimbali hawapo (pichani) katika Jengo jipya la Kituo cha Amani na Usalama kilichopewa jina Rasmi la Mwalimu Julius Nyerere, Addis Ababa nchini Ethiopia.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kutangazwa rasmi kwa Jina la Mwalimu Julius Nyerere katika kituo hicho cha Amani na Usalama.

Makonda akabidhiwa jengo la Mwananyamala, asema kwanini anajiweka karibu...


Balanced the Books - Joel Osteen


Mbowe atembelea shamba lake lililopigwa marufuku na Serikali




Mbowe akiwa shambani kwake leo wilayani Hai
By Mwandishi Wetu, Mwananchi

Hai. Mwenyekiti wa Chadema ambaye pia ni Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe ametembelea shamba lake la kilimo cha kisasa cha mboga mboga ( Green House) yaliyopo Hain na kuwajulia hali wafanyakazi pamoja na wataalam wake leo Ijumaa.

Pia, Mbowe amepata wasaa ya kuzungumza na baadhi ya wafanyakazi ambao walimweleza hofu kubwa waliyoingiwa nayo ya kupoteza ajira zao wanazozitegemea katika kuendesha maisha yao ya kila siku.

Hali hiyo imekuja baada ya Mkuu wa Wilaya ya Hai, Gellasiu Byakanwa kupiga marufuku shughuli za kilimo zinazoendeshwa na shamba la Kilimanjaro Veggies linalomilikiwa na Mbowe.

Byakanwa alitoa amri hiyo baada ya kutembea shamba hilo lenye ukubwa wa hekari mbili akisema kilimo hicho ni kinyume cha sheria kwani shamba hilo lipo ndani ya mita 60 kutoka mto Weruweru.

Mchakato ujenzi wa reli ya umeme Dar – Moro waanza


By Peter Elia, Ephrahim Bahemu mwananchipapers@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Rais John Magufuli amesema Serikali imeanza kupitia zabuni ili kumpata mkandarasi kwa ajili ya ujenzi wa reli ya kisasa (Standard Gauge) kutoka Dar es Salaam mpaka Morogoro, umbali wa kilomita 200.

Amesema treni zitakazopita katika reli hiyo zitatumia mafuta na umeme na mradi huo utasaidia pia kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam.

Sambamba na mradi huo, amesema Serikali itajenga barabara ya haraka ya njia sita, (Express Road) kutoka Dar es Salaam hadi Chalinze.

“... Hatua zote zimekamilika na kilichobaki ni mazungumzo na makandarasi kabla ya kuanza kujenga,” alisema Rais Magufuli.

Ajali ya Basi na Lori la Mbao Yaua na Kujeruhi 32 Iringa


Mtu mmoja amefariki dunia na wengine 32 kujeruhiwa vibaya baada ya basi la Vitu Laini linalofanya safari zake kutoka vijiji vya Kilolo kwenda Iringa Mjini kugongana na lori la mbao karibu likiwa limekaribia kufika Iringa Mjini.

Moto unaendelea kuteketeza makazi ya askari Moshi


Moto ukiteketeza makazi ya Askari wa Kikosi cha
By Daniel Mjema,Mwananchi

Moshi. Moto mkubwa ambao chanzo chake bado hakijafahamika, unaendelea kuteketeza jengo la ghorofa mbili la makazi ya Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) la mjini Moshi usiku huu.

Vikosi vya zimamoto na uokoaji kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Moshi na Kiwanda cha Sukari cha TPC vilikuwa vikiendelea na jitihada za kuuzima moto huo.

Mashuhuda wameliambia gazeti hili kuwa moto huo umeanza saa 2: na hadi kufikia saa 4:00 ulikuwa umeteketeza ghorofa ya pili unakosadikiwa kuanzia.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa familia zote za askari wa kikosi hicho cha FFU wanaoishi katika nyumba hiyo wamefanikiwa kutoka salama isipokuwa baadhi ya mali zimeteketea.

Mwandishi wa habari hizi ameshuhudia jitihada kubwa zikifanyika za kuuzima moto huo lakini unaonekana kuzidi kushika kasi baada ya gari la Halmashauri kuishiwa maji.

Hii ni mara ya pili kwa jengo hilo kuungua moto, miaka ya hivi karibuni lililipuka moto na vikosi vya zimamoto vilifanikiwa kuudhibiti.

Dakika 20 za Rais Magufuli kwenye uzinduzi wa mradi wa mwendokasi


Hotuba ya Rais Magufuli kumkaribisha Tanzania Rais wa Uturuki


KICHUPA CHA LEO SHOLO MWAMBA GHETTO Official Music Video YouTube


WAZIRI NCHEMBA AONGOZA ZOEZI LA UTEKETEZAJI SILAHA HARAMU 5,608 MKOANI KIGOMA


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba akikagua silaha haramu zilizoandaliwa kwa ajili ya kuteketezwa wakati wa zoezi la uteketezaji wa Silaha hizo lililofanyika mkoani Kigoma ambapo jumla ya Silaha haramu 5,608 zimeteketezwa na Jeshi la Polisi ikiwa ni juhudi za Serikali katika kupambana na uzagaaji wa Silaha haramu hapa mchini ambazo zimekuwa zikitumika katika matukio mbalimbali ya kihalifu.
Silaha haramu zikiwa zimepangwa katika uwanja wa Lake Tanganyika tayari kwa uteketezaji wakati wa zoezi hilo lililofanyika mkoani kigoma ambapo jumla ya Silaha haramu 5,608 zimeteketezwa na Jeshi la Polisi ikiwa ni juhudi za Serikali katika kupambana na uzagaaji wa Silaha haramu hapa mchini ambazo zimekuwa zikitumika katika matukio mbalimbali ya kihalifu.

Manara Atangaza Kumposa Wema Sepetu


Haji Manara (Kushoto), Wema Sepetu (Kulia).
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Haji Sunday Manara amelipa mtihani mwingine Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kuahidi kufanya maamuzi makubwa endapo ratiba ya ligi kuu haitabadilishwa hadi mwisho wa msimu.
Maamuzi ambayo Haji ametangaza kuyafanya ni kumposa mrembo wa Tanzania (Miss Tanzania) mwaka 2006 Wema Sepetu na kumuoa endapo atakubali, lakini kama hatakubali, Haji ameahidi kutembea akiwa amevaa nguo ya ndani pekee (Boxer) kutoka nyumbani kwake hadi katika ofisi za TFF zilizoko Ilala Dar es Salaam.
“Nimalizie Kwa kuwapa mtihani mwingine TFF na bodi ya Ligi, iwapo Kama ratiba yao ya Ligi kuu na Kombe la shirikisho haitabadilishwa kuanzia sasa hadi mwisho wa msimu, ntamposa mlimbwende Wema Sepetu, na akikubali ntamuoa, akikataa ntatembea na boxer toka Nyumbani kwangu hadi TFF” Amesema Manara

WITO KWA WALIOKUWA WAFANYAKAZI WA MGODI WA DHAHABU BULYANHULU WALIOPIMWA AFYA KATIKA HOSPITALI YA MUHIMBILI


WITO KWA WALIOKUWA WAFANYAKAZI WA ULIOKUWA MGODI WA DHAHABU BULYANHULU

UPIMAJI ULIOFANYIKA HOSPITALI YA MUHIMBILI
Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) unawakaribisha walioorodheshwa hapo chini kufika katika ofisi za OSHA zilizopo Kinondoni Manyanya karibu na mahakama kati ya tarehe 26 na 27 Januari ili waweze kupewa majibu yao. Tangazo hili linawahusu waliopimwa Muhimbili tu. Waliopimwa Bugando wanaombwa kusubiri tangazo jingine

BI.TUMAINI LEMA ANATAFUTWA ATAKAYEMUONA ATOE TAARIFA POLISI


Bi.Tumaini Lema (pichani) anatafutwa kwa tuhuma za wizi akiwa mtumshi wa dukani katika maeneo ya Kakola mgodini,mkoani Shinyanga taarifa zimetolewa polisi kwa namba hii Bug/RB/64/17 , yeyote atakayemuona mtuumiwa huyu Bi.Tumaini Lema atoe taarifa polisi na akamatwe mara moja. Ahsanteni

President Kenyatta lauds diaspora for contribution to economic growth



President Uhuru Kenyatta and Indian Prime Minister Narendra Modi during their bilateral talks in New Dehli on Wednesday, January 11, 2017 flanked by government officials from both sides. PHOTO/PSCU

President Uhuru Kenyatta has applauded the role played by the Kenyan diaspora in economic growth, assuring them of his government’s facilitation in their stay abroad. The president said remittances from Kenyans living abroad hit the Ksh1.6 billion mark in 2015.

“Today, the Kenyan diaspora is contributing to our economy more than what tea and coffee are contributing to the exchequer,” President Kenyatta said.

The Head of State was speaking in New Delhi during a meeting with the Kenyan diaspora in India.
President Kenyatta said his Administration has put in place a national diaspora policy that provides a roadmap for their involvement in the realization of the country’s development goals in line with Vision 2030.

Rais Magufuli apigilia msumari kwa wapiga dili nchini


Rais John Magufuli akihutubia wananchi wa Maswa kabla ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa wa Barabara ya Mwigumbi-Maswa, mkoani Simiyu. (Picha na Ikulu).
RAIS John Magufuli ameendelea kupigilia msumari kwa watanzania na viongozi wasiopenda kujishughulisha na kuwajibika na kutegemea zaidi fedha za bure za umma.

Amehakikishia kuwa hali zao zitaendelea kuwa mbaya, isipokuwa kwa wale watakaowajibika na kujishughulisha.

Amesema wale wote wanaolalamika kuwa hawana fedha mfukoni kwa hivi sasa, walizokuwa nazo hazikuwa zao, ndio maana wanalalamika.

Katika hotuba zake mwaka jana katika sehemu mbalimbali nchini, Rais alisema wanaolalamika hawana hela mfukoni ni ‘wapiga dili’.

Rais alibainisha kuwa Serikali ya Awamu ya Tano, itahakikisha inamaliza hali mbaya iliyokuwa inalikumba taifa la watanzania, ambapo watu wachache ndio waliokuwa wakinufaika na fedha za umma huku wananchi wengi wakiendelea kuumia na umasikini.

Ni marufuku kuuza mapanga, mishale barabarani, Sirro


RAIS DKT. MAGUFULI AHUTUBIA WANANCHI WA SHINYANGA KATIKA KILELE CHA MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA MIAKA 53 MAPINDUZI YA ZANZIBAR


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono kuwasalimia wananchi wa Shinyanga waliofika katika uwanja wa mpira wa Kambarage katika kilele cha Maadhimisho ya Sherehe za miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar mkoani humo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Shinyanga katika kilele cha maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Kambarage mkoani humo.

Hakuna chakula cha msaada -Magufuli


Rais John Magufuli akikata utepe akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka pamoja na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa kuashiria ufunguzi wa barabara ya Bariadi-Lamadi yenye kilometa 71.8. (Picha na Ikulu).
RAIS John Magufuli amesema inawezekana asiwe mwanasiasa mzuri, lakini siku moja atakumbukwa kwa mambo ambayo anayafanya, kwa sababu dhamira yake ni nzuri katika kusimamia ubadhirifu wa fedha za umma na kusimamia miradi ya maendeleo ili watanzania wote wanufaike.

Pia amesisitiza kuwa serikali haitatoa chakula cha msaada kwa wananchi. Aidha, katika kusimamia kauli zake mkoani Simiyu, Rais Magufuli ameagiza hospitali ya rufaa ya mkoa wa Simiyu ambayo aliweka jiwe la msingi, ujenzi wake jana kujengwa kwa Sh bilioni 10 na kukataa kiwango kilichokuwa kimekadiriwa cha Sh bilioni 46.

Rais Magufuli alitoa kauli hiyo jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Somanda wilayani Bariadi, kabla ya kwenda kuzindua ujenzi wa barabara.

Awali Rais alikuwa na mikutano mingine katika vijiji vya Nyashimo, Masanzakona, Lamadi na Nyamikoma wilayani Busega mkoani Simiyu katika siku ya kwanza ya ziara yake mkoani humo.

“Nimeweka jiwe la msingi katika ujenzi wa hospitali, ujenzi wake wamesema ni Shilingi bilioni 46, nimesema kitu hicho hakiwezekani, tena wamekosea sana kuniita mimi kuja kuweka jiwe la msingi,” alisema Rais Magufuli.

Kesi ya Mke wa Bilonea Msuya Yaahirishwa Tena


DAR ES SALAAM: MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu inatarajiwa kutoa uamuzi wa kumwachia  ama kutomwachia huru mke wa marehemu bilionea Erasto Msuya aitwaye Miriam Mrita (41) na mwenzake ambaye ni mfanyabiashara, Revocatus  Muyela (40), wanaotetewa na mawakili Peter Kibatala na John Mallya  ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Januari 23 mwaka huu.

Uamuzi huo ulitolewa leo mahakamani hapo kutokana na upande wa serikali kushindwa kubadilisha hati ya mashtaka ya kesi hiyo ndani ya siku mbili kama ilivyoamliwa Januari 9, mwaka huu.
 Januari 9, 2017 Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa, aliuamuru upande wa serikali kubadilisha hati ya mashitaka ndani ya siku mbili ambapo   alisema uamuzi huo  unatokana na kupitia hoja za pande zote mbili na kubaini kuwa hati ya mashitaka ilikuwa na mapungufu mawili likiwemo la kutoonyesha kama kuna mtu ambaye amesababisha kifo kwa mtu mwingine.

Mmiliki gesti anyweshwa, aibiwa


Image result for Mbilinyi Guest House SUMBAWANGA
POLISI mkoani Rukwa inawasaka wageni waliofikia katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Mbilinyi Guest House iliyopo katika manispaa ya Sumbawanga kwa tuhuma za kumwibia mmiliki wa nyumba hiyo vitu na fedha taslimu, vyote vikiwa na thamani ya Sh 914,000 baada ya kumnywesha.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa , George Kyando amesema wizi huo ni wa Januari 9, mwaka huu saa mbili usiku katika nyumba hiyo ya kulala wageni ya Mbilinyi.

Amemtaja mmiliki wa nyumba hiyo ambaye pia ni mkazi wa eneo la Majengo, manispaa ya Sumbawanga kuwa ni Tumain Mbilinyi (32) ambaye aliibiwa TV mbili za nchi 24 za thamani ya Sh 600,000 na fedha taslimu Sh 314,000 na watu ambao walikuwa ni wapangaji katika nyumba hiyo.

“Uchunguzi wa awali wa kipolisi umebaini kuwa watu hao waliokuwa wamepanga vyumba katika nyumba hiyo ya kulala wageni waliwapatia vimiminika vinavyosadikiwa kuchanganywa na dawa za kulevya mhudumu wa nyumba hiyo, mlinzi na mhudumu wa kike wa baa ya Uyole," amesema Kamanda.

Kamanda alisema mhudumu huyo wa baa ya Uyole ndiye aliyeenda na watuhumiwa hao katika nyumba hiyo ambapo waliwanywesha hadi kulewa na kutumia mwanya huo kuiba vitu hivyo vya thamani ya Sh 914,000.

Kyando aliwataka wahudumu na walinzi wote wa mahoteli, baa na nyumba za kulala wageni kuwa makini na kuacha tabia ya kupokea vyakula, vinywaji au kitu chochote wawapo kazini hasa kwa watu wasiowafahamu.

Alisema watuhumiwa hawajakamatwa na jitihada za kuwasaka zinaendelea ili wakikamatwa sheria ichukuwe mkondo wake.

HABARI LEO

Nape ampongeza Diamond kutumbuiza Afcon

 amNapepongeza Diamond kutumbuiza Afcon

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (kushoto) akimkabidhi bendera ya Taifa, Diamond Platnumz katika hafla ya kumuaga iliyofanyika Dar es Salaam jana. Msanii huyo anakwenda Gabon kutumbuiza ufunguzi wa mashindano ya Afcon yatakayoanza keshokutwa. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice-Tanzania, Salum Salum na mchekeshaji Joti. (Picha na Cosmas Mlekani).
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amempongeza mwanamuziki wa Tanzania, Nassib Abdul ‘Diamond Platnumz’ kwa kupata nafasi ya kutumbuiza kwenye ufunguzi wa fainali za Mataifa ya Afrika, Afcon.

Michuano hiyo itakayofanyika Gabon inatarajiwa kuanza keshokutwa hadi Februari 5 mwaka huu ambapo mataifa 16 yatashiriki.

Nape akizungumza katika hafla ya kumkabidhi bendera ya taifa Diamond Dar es Salaam jana, alisema kitendo cha msanii huyo kwenda kutumbuiza katika ufunguzi huo ni heshima kubwa kwa Tanzania.

Alimtaka Diamond kwenda kuliwakilisha vizuri taifa licha ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, kutopata nafasi ya kushiriki fainali hizo.

RAIS DKT. MAGUFULI AWASALIMIA WAKAZI WA CHATO MJINI, PIA ATEMBELEA SHULE YA MSINGI ALIYOSOMA CHATO


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika benchi la kibanda cha kupigia kiwi (Shoe Shine) pamoja na wakazi wengine wa Chato katika eneo maarufu kama Stendi za zamani Chato mkoani Geita. Kibanda hicho cha Kiwi ndicho Rais Dkt. Magufuli alichokuwa akisafishiwa viatu  vyake kabla ya kuwa Rais, pia ni sehemu ambayo alikuwa akipenda kukaa na  kubadilishana mawazo na wakazi wa Chato wakati akiwa mapumzikoni kipindi cha Nyuma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Chato mkoani Geita. Shule hiyo ya Msingi Chato ndiyo Rais Dkt. Magufuli alisoma kuanzia darasa la kwanza mpaka Darasa la Saba. Rais Dkt. Magufuli amewaasa Wanafunzi hao kusoma kwa bidii kwasababu yeye pia alisoma shuleni hapo. Picha na Mpigapicha Maalum.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Chato mkoani Geita. Shule hiyo ya Msingi Chato ndiyo Rais Dkt. Magufuli alisoma kuanzia darasa la kwanza mpaka Darasa la Saba. Rais Dkt. Magufuli amewaasa Wanafunzi hao kusoma kwa bidii kwasababu yeye pia alisoma shuleni hapo. Picha na Mpigapicha Maalum.