Mchakato ujenzi wa reli ya umeme Dar – Moro waanza


By Peter Elia, Ephrahim Bahemu mwananchipapers@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Rais John Magufuli amesema Serikali imeanza kupitia zabuni ili kumpata mkandarasi kwa ajili ya ujenzi wa reli ya kisasa (Standard Gauge) kutoka Dar es Salaam mpaka Morogoro, umbali wa kilomita 200.

Amesema treni zitakazopita katika reli hiyo zitatumia mafuta na umeme na mradi huo utasaidia pia kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam.

Sambamba na mradi huo, amesema Serikali itajenga barabara ya haraka ya njia sita, (Express Road) kutoka Dar es Salaam hadi Chalinze.

“... Hatua zote zimekamilika na kilichobaki ni mazungumzo na makandarasi kabla ya kuanza kujenga,” alisema Rais Magufuli.

No comments:

Post a Comment