Tofauti ya kuwa na virusi vya Ukimwi na kuwa na Ukimwi

HIV-patient

Wasomaji wengi wa safu hii wamekuwa wakiniuliza nini tofauti kati ya kuwa na virusi vya Ukimwi na mtu kuwa na Ukimwi.Ukweli ni kwamba kuna tofauti kati ya mtu mwenye virusi vya Ukimwi na yule ambaye ana Ukimwi, jambo ambalo wengi hawalijui.
Mtu anapokuwa ameambukizwa virusi vya Ukimwi haanzi kuugua mara moja na badala yake huweza kuishi na virusi hivyo kwa muda mrefu hata zaidi ya miaka 10 bila kuonesha dalili zozote.
Tofauti yake na mtu mwenye Ukimwi ni kwamba huyu ambaye anatajwa kuwa anao dalili za magonjwa nyemelezi hujitokeza haraka kutokana na kinga yake ya mwili kupungua kupita kiasi kutokana na kuharibiwa na virusi.
Magonjwa ambayo yatajitokeza ni pamoja na kuharisha, kuvimba tezi mbalimbali mwilini mwake hasa shingoni, kukohoa, kutokwa na malengelenge ya neva za ngozi au kupatwa na mkanda wa jeshi au kuwa na utando mweupe mdomoni.
Hata hivyo, siyo kila anayeumwa maradhi hayo tuliyoyataja hapo juu ni mwathirika wa Ukimwi, hujulikana kuwa ameathirika baada ya kupimwa na kuthibitishwa kwa vipimo.
MTU ANAAMBUKIZWAJE UKIMWI?
Bahati nzuri wengi siku hizi wanajua jinsi Ukimwi unavyoambikizwa. Kuna njia nyingi za mtu kuweza kuambukizwa Ukimwi lakini hapa kuna nne muhimu.
Virusi vya Ukimwi huishi kwenye majimaji kama vile yale yaliyo sehemu za siri za mwanamke, mbegu za kiume, maziwa ya mama, majimaji ya vidonda, usaha, damu na kadhalika.
Lakini majimaji haya huhitaji njia ya kupita ili maambukizi yatokee. Hivyo basi, mtu anaweza kuambukizwa VVU akiguswa na majimaji ya mwenye Ukimwi kupitia kujaamiiana kwa njia ya kawaida na kinyume cha maumbile au kwa njia ya mdomo (oral sex), hasa kama atakuwa amechubuka sehemu za siri.
Pili, mama mzazi anaweza kumuambukiza mtoto wake Ukimwi wakati akiwa tumboni, wakati wa kujifungua au akiwa anamnyonyesha.
Tatu, mtu anaweza kuambukizwa Ukimwi kwa kupewa damu iliyo na Virusi Vya Ukimwi (VVU) na nne kwa kuchangia sindano au nyembe ambazo zimetumika na mtu mwenye maambukizo.
Takwimu zilizotolewa na Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi zinaonesha kuwa maambukizi kwa njia ya kujamiiana na mtu mwenye maambukizi ni asilimia 82.1. Maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kwa njia ya kunyonyesha au wakati wa kujifungua ni asilimia 5.9.
Wanaopata maambukizi kutokana na kuongezewa damu yenye virusi vya Ukimwi ni asilimia 0.3 wakati wanaokumbwa na maradhi hayo kwa njia nyingine kama vile kuchangia sindano, nyembe ni asilimia 1.7. na wale ambao wanapata Ukimwi bila kufahamu chanzo ni asilimia 10.
Ni vyema wasomaji wakafahamu njia ambazo haziambukizi kabisa Ukimwi. Mtu hawezi kuambukizwa kwa kuumwa na mbu au kwa kupiga chafya au kukohoa kunakofanywa na mwenye virusi vya Ukimwi.
Mtu hapati maradhi hayo kwa kula, kulala kitanda kimoja, kuogelea bwawa moja, kutumia vikombe au sahani moja kwa chakula au kuchangia choo na mtu mwenye virusi vya Ukimwi.
USHAURI
Mtu aliye na Ukimwi inatakiwa apate mahitaji muhimu ya lishe na jamii ifundishwe kuachana na tabia ya kuwanyanyapaa au kudhani kuwa aliye na Ukimwi ni mzinifu au amekosa maadili.

Zari ahofia kuishi Bongo!

zariiiStori: MUSA MATEJA, WIKIENDA
Dar es Salaam: Ubuyu! Tumbuatumbua ya majipu ya Rais wa Awamu ya Tano, Dk. John Pombe Magufuli ‘JPM’ inadaiwa kumtisha mwandani wa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kuja kuishi Bongo ikidaiwa kisa ni utajiri mkubwa alionao wenye shaka juu ya malipo ya ushuru na mapato.
Habari kutoka kwenye chanzo cha ndani cha familia ya Diamond, zimeeleza kuwa Zari alikuwa na mpango wa kuhamishia miradi na makazi yake rasmi Dar mwanzoni mwa mwaka 2016 lakini ndoto hiyo inaonekana kuyeyuka.
Chanzo hicho kilieleza kuwa, familia ya Diamond imekuwa ikimshinikiza jamaa huyo amshawishi Zari kuwekeza Bongo lakini kwa sasa mpango huo umefutika kwani mwanadada huyo anaogopa kutumbuliwa majipu.
zari1
“Unajua Zari anafuatilia kila kitu kinachoendelea nchini. Kwa hiyo usidhani hajui mambo ya TRA (Mamlaka ya Mapato) yalivyochachamaa.
“Unajua anasema akihamia Bongo itabidi aingize nchini yale magari yake ya kifahari anayotembelea akiwa Sauz (Afrika Kusini) au Uganda lakini anahofia tumbua majipu ya Magufuli.
“Wewe fikiria kama lile Range (Rover) la Wema (Sepetu) limekamatwa na TRA, itashindikana nini kukamata Hummer au Lamborghini ya Zari?
“Nafikiri ishu ni utajiri wake. Nilishasoma kwenye vyombo vya habari vya Uganda kuwa utajiri wake wa ghafla umekuwa ukiibua sana maswali na yeye huwa hapendi kuzungumzia vyanzo vya utajiri wake,” kilinyetisha chanzo chetu.
ZARI47817Baada ya kumwagiwa ubuyu huo, mwanahabari wetu alithibitisha kuwa kweli Zari hayupo Bongo yupo Sauz hivyo alimsaka Diamond ambaye alikuwa na haya ya kusema: “Zari ana miradi mingi, muda wa kuwekeza Bongo ukifika atakuja kufanya hivyo.
uhusu mheshimiwa (Magufuli) mimi nampongeza kwa kutumbua majipu kwa sababu tulikuwa tunahitaji kiongozi kama yeye,” alisema Diamond na kuongeza kuwa mpango wa Zari wa kuja kuishi Dar upo palepale.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA RUFAA YA MAWENZI MKOANI KILIMANJARO.


Waziri mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Majaliwa Kassim Majaliwa akiwasili Ikulu ndogo ya mjini Moshi.
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akisalimiana na Waziri mkuu  Majaliwa.
Waziri Mkuu  akislimiana na Mstahiki meya wa  Manispaa ya Moshi,Raymond Mboya .

WANANCHI WATAHADHARISHWA JUU YA HOMA YA ZIKA


Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii, Watoto na Wazee Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na Waandishi wa Habari Mijini Dodoma (Hawapo Pichani)  akitoa tamko la Wizara juu ya ugonjwa wa homa ya Zika kushoto ni Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Dodoma Dkt Zainabu Chaula. Picha Na Raymond Mushumbusi Maelezo

Na Raymond Mushumbusi Maelezo
Wananchi wa Tanzania watahadharishwa juu ya ugojwa wa  homa ya Zika uliripotiwa kutokea katika nchi za Amerika ya kusini hivi karibuni.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo  Mijini Dodoma na Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii, Watoto na Wazee Mhe. Ummy Mwalimu alipokuwa akitoa tamko juu ya uvumi ulioenea kuhusu homa ya Zika iliyoenea katika nchi za Amerika ya kusini.
Mhe.Ummy Mwalimu amewaasa watanzania kuwa na tabia ya kwenda hospitali kila wanapojisikia dalili za homa na kupima kwani sio kila homa ni malaria kwani dalili za homa ya malaria zinafanana kabisa na dalili za ugonjwa wa homa ya Zika.
“ Nawaomba ndugu zangu watanzania tuzingatie usafi ili kuzuia mazalia ya mbu kwani ugonjwa huu unatokana na virusi vinavyoenezwa na mbu na hao mbu wanapatikana sana nyakati za asubuhi mchana na jioni hivyo nawasihi kutumia dawa za kuua mbua na vyandarua wakati wa kulala.”

Mkoa wa Dar es Salaam Sasa Kuwa na Wilaya Tano


RAIS Dk. John Magufuli ameidhinisha kuwepo kwa wilaya tano katika jiji la Dar es Salaam, badala ya tatu zilizokuwepo awali, ili kuleta maendeleo ya haraka hususan katika elimu. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki, alisema jana kuwa, waliwasilisha ombi la ugawaji wa wilaya za Kinondoni na Temeke kwa rais, ambapo ameshaliidhinisha.

Serikali yatoa taarifa kuhusu ugonjwa wa homa ya Zika.

 1. Utangulizi Kumekuwepo na taarifa kupitia vyombo mbalimbali vya habari vya Kitaifa na Kimataifa kuhusu Homa ya Zika ambao ni ugonjwa unaosababishwa na kirusi kijulikanacho kama “Zika Virus”.&nbs...
Read More

HALI HALISI YA LANGO KUU LA KUINGILIA UWANJA WA CCM KIRUMBA JIJINI MWANZA.

Mwonekano katika lango Kuu la Kuingilia katika Uwanja wa mpira wa CCM Kirumba Jijini Mwanza pindi mvua inaponyesha. Ni zaidi ya Usumbufu, kero na adha kwa wanaoingia na kutoka Uwanjani hapo pindi mvua inaponyesha.
Ni zaidi ya Usumbufumbu kwa mashabiki wa mpira pindi mvua inaponyesha wanapokuwa wakiingia amba kutoka Uwanjani, katika Uwanja wa CM Kirumba Jijini Mwanza kutokana na maji kutuama katika barabara inayoingia na kutoka katika lango Kuu la kuingilia Uwanjani hapo.
Wahusika mlione hili kama changamoto inayopaswa kutafutiwa utatuzi.
Picha na George Binagi-GB Pazzo Wa BMG.

TAZAMA VIDEO YA WEMA NA IDRIS WALIPOHOJIWA CLOUDS FM NA DIVA

Wema Sepetu na Idris Sultan wamekuwa gumzo wiki hii baada ya kuweka hadharani rasmi uhusiano wao uliokuwa ukifahamika kama tetesi tu kwa muda mrefu.
Couple ya ‘Wedris’ ilipata nafasi ya kuhojiwa exclusive na mtangazaji wa Clouds Fm, Diva kwenye kipindi cha Ala Za Roho usiku wa Alhamisi (Jan 28), ambapo kila mmoja alifunguka mambo mengi kuhusu toka walipokutana na kuanza kupendana, kuhusu wema alivyogundua kuwa ameshika ujauzito wa Idris na mambo mengine.
Kama hukupata bahati ya kusikiliza tazama hapa sehemu ya mahojiano hayo walipokuwa studio za Clouds Fm.

RAIS MAGUFULI AMUONGEZEA MKUU WA MAJESHI, JENERALI MWAMUNYANGE MWAKA MMOJA

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Pombe Magufuli, amemuongezea Mkuu wa Majeshi wa Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange mwaka mmoja wa kuendelea kuliongoza Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).Picha kutoka Maktaba)

[VIDEO] Tanzanian man arrested after hiding girlfriend in a pit for over eight months

Posted by  

hidden-pit
Print Friendly
A man in Tanzania has been arrested after reportedly hiding his girlfriend in a cement pit for more than 8 months.
The man is reported to have kept the woman in a bid to use the woman in a ritual intended to bring him wealth.
The man’s neighbors tipped the Tanzanian police after they suspected that there was a human being in the pit.
The woman, said to be in her twenties told her rescuers that she used to survive on just two meals a week.
Video Player
00:00
01:39

Kidum ft Juliana Kanyomozi - Haturudi Nyuma


Wema Chini ya Ulinzi

wema33
STORI: Mwandishi Wetu, Risasi Jumamosi
DAR ES SALAAM: Mama kijacho Wema Abraham Sepetu ‘Madam’ kwa mara nyingine ametengeneza kichwa cha habari, safari hii amewekwa chini ya ulinzi wa polisi kwa kosa la kuendesha gari aina ya Range Rover Evogue bila kuwa na vibali, Risasi Jumamosi lina ‘full’ stori.
Tukio hilo lililodumu kwa takriban saa tatu lilijiri Jumanne iliyopita maeneo ya Aficana, Mbezi Beach jijini Dar wakati mrembo huyo alipokuwa ‘kiguu na njia’ kwenda kwenye bethidei ya rafiki yake aliyefahamika kwa jina la Kibadude.
index3NI LILE ALILODAI KUJIZAWADIA
Kwa mujibu wa chanzo makini kilichokuwepo eneo la tukio, gari hilo alilokamatwa nalo Madam ni lile alilojizawadia kwa mbwembwe nyingi mwishoni mwa mwaka jana katika siku yake ya kuzaliwa ambalo lina thamani ya shilingi milioni 200 za Kibongo.
“Nimepiga picha. Wamemtaiti hapa Mbezi Africana, naona maofisa wa TRA wanamhoji. Lina tatizo katika uhalali wa kuingia nchini. Hapa sasa naona wanaomhenyesha ile mbaya. Si kawaida.”
index5AMWAGA CHOZI
“Sasa namuona Madam machozi yanamtoka yenyewe… anahaha, mara aende huku mara kule. Nahisi so litakuwa limemkalia vibaya maana kila simu anayopiga hapati msaada,” kilinyetisha chanzo hicho.
index2TRA WABAINI FIGISUFIGISU
Gazeti hili lilizungumza na ofisa mmoja wa TRA ambaye alikuwepo kwenye tukio hilo aliyeomba hifadhi ya jina kwa kuwa si msemaji wa mamlaka hiyo aliweka wazi kuwa, walibaini figisufigisu katika gari hilo.
gari la wema“Hili gari ni moja kati ya magari ambayo yanaingia nchini kutokea nchi ya Msumbiji. Hata namba zake za usajili zinaonesha hivyo. Sasa huwa yanakatiwa vibali vya miezi mitatu au kulipiwa ushuru na kununuliwa. Liliingia nchini tangu mwaka jana.
“Tumekuta halina vibali maana vibali vya miezi mitatu vimeisha, tumemuuliza atoe nyaraka za gari, anasema zipo nyumbani, tukamwambia twende huko nyumbani ukazitoe, akabadili lugha, akasema anazo Steve (Nyerere). Inaonekana hili gari lina matatizo makubwa ya ushuru,” alisema ofisa huyo.
indexFIGISU NYINGINE
Kumbukumbu zinaonesha gari hilohilo la Wema ambalo alisema amejinunulia kwa fedha zake, ndilo alilodaiwa kununuliwa na mbunge machachari wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye aliwahi pia kutajwa kuwa ndiye baba kijacho wake kabla ya Idris Sultan kuibuka na kujinadi kuwa ndiye ‘mmiliki’ halali wa tumbo hilo.
inde6xKIGOGO SERIKALINI AMUOKOA
Paparazi wetu alimtafuta mtu wa karibu kabisa na Wema ambaye alieleza kuwa, Madam baada ya kuhaha kwa muda mrefu eneo hilo huku akiwa chini ya ulinzi wa polisi wenye bunduki, alipata wazo la kumpigia kigogo mmoja serikalini (jina tunalo) ambaye alimpa msaada kwa masharti.
“Alimpigia simu… (anataja jina la kigogo), akamweleza matatizo yaliyomkuta, naye akazungumza na maofisa wa TRA, wakakubaliana kwa masharti kwamba asilitumie gari hilo ndani ya wiki moja mpaka apeleke vibali vya gari hilo,” alisema mtu huyo wa karibu na Wema.
HUENDA LIKATAIFISHWA KAMA LA WOLPER
Kwa mujibu wa taratibu na sheria za TRA, endapo Wema atashindwa kutoa nyaraka muhimu za gari hilo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake ikiwa ni pamoja na  kutaifishwa kwa gari hilo kama ilivyomtokea mwigizaji Jacqueline Wolper ambaye mwaka 2014, gari lake aina ya BMW X6 lilikamatwa na kutaifishwa kwa kushindwa kulipia ushuru na kukosa vibali halali.
WEMA ASAKWA
Baada ya kupewa taarifa hizo, gazeti hili lilimtafuta Wema kwenye simu yake ya mkononi lakini muda wote iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi, hakujibu.
MENEJA WA WEMA ANENA
Alipoulizwa kuhusu suala hilo, meneja wa msanii huyo, Martin Kadinda alisema yeye alisikia kwa watu kuhusu taarifa za Madam kukamatwa na gari hilo lakini alipomuuliza alimwambia si kweli, ni uzushi tu na hata gari hilo lipo nyumbani aende kuliona jambo ambalo alilifanya na kweli akajionea gari hilo.
“Ni uzushi tu. Nimeongea na Madam, akanihakikishia kwamba hamna kitu kama hicho. Nikaenda kulitazama gari, nikalikuta nyumbani kwake Ununio, shwari kabisa,” alisema Martin.
Gazeti ndugu na hili, Amani, toleo la Alhamisi iliyopita, ukurasa wa nyuma kulikuwa na habari yenye kichwa; Range la Wema layeyuka. Msingi wa habari hiyo ni taarifa kuwa, Wema haonekani akiwa na gari hilo licha ya kujinadi kuwa ni lake. Amekuwa akitumia kigari kidogo ‘ki-kirikuu’ kuendea kwenye shughuli zake.
Ilidaiwa kuwa, Wema alilipeleka gereji au yadi ya kuuzia magari, gari hilo hali iliyowafanya mapaparazi wa OFM kulisaka bila mafanikio huku ikielezwa kuwa, gari hilo si lake bali huwa anapepewa kwa muda kujiachia nalo.

Wema Sepetu Afunguka ya Moyoni Kuhusu Penzi Lake kwa Idris

Ikiwa leo Idris Sultan anasherekea miaka yake kadhaa ya kuzaliwa, mpenzi wake Wema Sepetu amefunguka haya kwenye ukurasa wake mtandaoni kuonyesha dunia ni jinsi gani alivyozama penzini kwa kijana huyo ambaye ni mshindi wa BBA 2014.

Waziri Mkuu: Tutahakikisha Nidhamu Inarudi Serikalini

Waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa,amesema serikali imeweka msisitizo katika kuhakikisha inarudisha nidhamu kwa watumishi wa umma kwa kuweka mkazo katika uadilifu, uwajibikaji, kutoa huduma kwa wakati. Waziri mkuu Majaliwa ameyasema hayo  katika mkutano wa pili kikao cha tatu Bungeni Mjini Dodoma alipokua akihitimisha hoja ya kujadili hotuba ya Rais John Magufuli aliyoitoa...
Read More

Diamond Ajinyakulia Tuzo Nyingine Kenya


Running Your Race


Wafungwa jela maisha kwa kusafirisha ‘unga’

By Daniel Mjema, Mwananchi


Moshi. Mahakama Kuu imewahukumu kifungo cha maisha jela, watu wawili baada ya kupatikana na hatia katika kesi mbili tofauti za kusafirisha dawa za kulevya zenye thamani ya Sh289.2 milioni.

Washtakiwa hao waliohukumiwa jana na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Moshi, Aishiel Sumari ni Hamis Suya, mkazi wa mkoa wa Tanga na Josephine Mumbi Waithera, raia wa Kenya.

Josephine alikuwa akishtakiwa kwa kusafirisha gramu 3,249.82 za dawa hizo aina ya heroini zenye thamani ya Sh146.2 milioni kwenda Vienna, Austria kupitia Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (Kia) wakati Suya alikamatwa akisafirisha gramu 3,191.3 za heroini zenye thamani ya Sh143 milioni kwenda jijini Arusha kwa Basi la Happy Nation.

Akitoa hukumu dhidi ya Suya, Jaji Sumari alisema upande wa mashtaka umeithibitishia Mahakama bila kuacha shaka kuwa

alikutwa na dawa hizo.

Alisema hakuna ubishi kuwa tembe 249 za heroini zikiwa ndani ya begi kwenye basi hilo lililokuwa likisafiri kati ya Dar es Salaam na Arusha Novemba 27, 2012 zilikuwa za mshtakiwa huyo.

“Hoja hapa ilikuwa nani ni mmiliki wa begi lile kati ya washtakiwa hawa watatu, yaani Mussa Mgonja, Suya na Abdulaziz Makuka, lakini kulikuwa hakuna ubishi begi la dawa zile lilikutwa ndani ya basi,” alisema Jaji Sumari. Alisema kitendawili hicho kiliteguliwa na maelezo ya Suya aliyoandika polisi na kukiri kosa hilo na kuwa aliyatoa kwa hiari yake bila kulazimishwa.

PICHA: ATHARI ZA MVUA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

 Vijana wakiwa wamekaa nje baada ya nyumba wanazoishi kujaa maji maeneo ya Jangwani jijini Dar es Salaam kufuatia mvua zilizonyesha leo.
 Kituo cha daladala za kwenda Gongolamboto cha Suwata Kariakoo kikiwa kimejaa maji hivyo  kuleta adha kwa watumiaji kufuatia mvuo hizo.

Testimony of Kenyan woman attacked by boyfriend with a hammer in Kansas

Posted by  

Elizabeth Kogo
Print Friendly
Elizabeth Kogo’s Testimony 5 yrs After Her Tragic Story that made National News in America
By Pastor Boniface Gitau
On January 23rd, 2011 a quiet neighborhood in Wichita, Kansas was struck by a tragic attempted homicide that caused chills to the residents that witnessed the aftermath or saw the news in the media. That afternoon, a young woman was fighting for her life after a vicious attack.
She was rushed to the hospital in a coma; the doctors tried all they could to save her life but gave up after failed resuscitation attempts. When all hope was lost, her mother in Kenya was sent documents to sign her off life support. But thank God for the tenacity of her loving caring mother who pleaded to God for the life of her precious daughter. She refused to sign the papers and believed God for a miracle.
This is the true story of Elizabeth Kogo whom God literally delivered her life from the jaws of death. It has now been 5 years since her dreadful attack. Although she still deals with the effects of TBI (Traumatic Brain Injury) and disabilities caused by the hammer that was lodged on her head, her resilient spirit has kept her going. She has defied all odds and through her determination and trust in God she went back to college to pursue a degree in social work at Wichita State University. She recently received a scholastic honor for her excellent academic achievement. Her hard work is finally paying off; she is set to graduate this Spring.
What is even more amazing about Elizabeth’s testimony is that nothing has deterred her from single handedly raising her son Florian as an unemployed full time student.
By God’s grace, she recently published a book, Delivered from the Jaws of Death. She talks about what exactly happened and the signs she overlooked that led her to stay in an abusive relationship. Her testimony is powerful and astounding. God has brought her this far to share with others her miraculous story of victory and triumph despite her tragedy. Her dreams may have been crushed but not shattered. At the point of death is where she found Jesus who restored her life and gave her an unspeakable joy, peace and divine purpose in life.
Elizabeth believes that indeed all things, even the bad things in life, work together for the good of those who love God. She has chosen to use her experiences to making a difference in the lives of others. Elizabeth still lives in Wichita, Kansa. She believes God will resurrect and fulfill her dreams in the same city where she almost lost her life. It takes great courage to confront one’s fears like she does. Reading her full storydocumented in her new book will inspire your faith in God who works wonders and miracles in the midst of the storms you may encounter.

Watuhumiwa 7 wa Makontena Ambao ni Wafanyakazi wa Bandari Waliokuwa Wametoroka Wakamatwa

Wafanyakazi saba kati ya wanane wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) waliotuhumiwa kuhusika kutorosha makontena 11,019 na magari 2,019 kutoka bandarini ambao walitoroka, wamepatikana na tayari wanaendelea kuhojiwa na polisi juu ya tuhuma hizo. Watumishi hao ni kati ya watuhumiwa 15 wa TPA waliotangazwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa kuwa wameshiriki...
Read More

Kisa Ujauzito, Wema Amuandikia Waraka Mzito Idris

Supastaa Wema Sepetu kupitia Instagram amempongeza mpenzi wake Idris kwa kumtengenezea historia katika maisha yake kwa kumpa ujauzito.

Hiki ndicho alichokiandika Wema Insta

Kwa hali hii Nchi inaliwa!

Makongoro oging’, AMANI

DAR ES SALAAM: Da! Wakati Rais John Pombe Magufuli ‘JPM’ akiendelea kutumbua majipu kwa vigogo mbalimbali serikalini, hasa wanaotuhumiwa kwa ufisadi, Amani limenasa vigogo wengine wanne wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambao wamejenga mahekalu ya mabilioni ya shilingi huku wakiishi maisha ya juu kama ‘miungu watu’, kweli nchi inaliwa! Awali, mahekalu mengine yaliyosemekana kuwa ni ya vigogo wa mamlaka hiyo, yalinaswa na kutolewa kwenye gazeti hili.
CHANZO CHAZUNGUMZA NA AMANI
Mapema wiki hii, chanzo chetu cha habari kilifika kwenye ofisi za gazeti hili na kuonana na wahariri wa Global Publishers kulalamikia maisha ya baadhi ya vigogo wa TRA kwamba ni ya anasa sana wakiwa wanaishi kwenye mahekalu (majumba) ya kifahari huku Watanzania walio wengi wanaishi kwa mlo mmoja tena kulala kwa kubanana.
MSIKIE MWENYEWE
“Jamani ndugu zangu, lengo la mimi kuja hapa ni kutaka kuwaambia kwamba, kuna vigogo wa TRA wanaishi Mbezi Beach. Wamejenga majumba ya kifahari. Wanamiliki magari ya kisasa, lakini najua pesa zao ni za ufisadi.
“Nimekuwa nikifuatilia kwenye vyombo vya habari ili kuona kama kuna siku watawekwa hadharani lakini wapi! Naamini serikali haijawajua. Wale wakifuatiliwa, watabainika namna walivyoitafuna hii nchi na ndiyo maana wanaishi kwa kuabudiwa hata na viongozi wa serikali ya mtaa.”
KWENYE VIKAO WANATUMA WAWAKILISHI
“Sisi wenye vijumba vya kujenga miaka saba havijaisha tunajisikia vibaya sana. Ni majirani zetu lakini hatuonani. Wakitoka nje ya mageti yao wamo ndani ya magari yenye tinted. Wananuka pesa hata familia zao. Wanaogopwa mtaani.
“Siku kukiwa na kikao cha serikali ya mtaa kuzungumzia mambo ya maendeleo wanatuma wadogo zao, shemeji zao, wengine wanatuma hata mahausigeli. Hivi ni haki kweli jamani?!”
IMG_1414KUONEKANA KWAO
“Mimi nimewahi kuwaona wawili tu kwa nyakati tofauti, walikuwa wana shida kwenye ofisi za serikali ya mtaa. Kusema ule ukweli nchi hii inaliwa sana. Kama kila mmoja angefanya mambo kulingana na kipato chake halali, taifa lingekuwa mbali sana. Lakini watu wanaiibia serikali kwa ajili ya kujitajirisha na familia zao,” alisema mtoa habari huyo.
KUNA DOGO WA MIAKA 27 NAYE
Wakati mtoa habari wetu akihitimisha hivyo, vyanzo vingine vya habari vimesema kuwa, kijana wa miaka 27 (jina linahifadhiwa kwa sasa), mfanyakazi wa kawaida (kama ‘mfagizi’) wa TRA anamiliki jumba la kifahari lenye vyumba vya kulala 10, sebule 2, vyoo vya umma vitatu, sehemu ya kulia chakula 2 huku msingi wa nyumba ukiwa na urefu wa nyumba nyingine.
“Huyu dogo ana miaka kama 27 tu, lakini anamiliki jengo la kifahari huko Goba. Maisha yake kwa ujumla ni ya kutumbua raha. Kumbe hawa jamaa wa TRA wana pesa sana. Mimi sikuwahi kufikiria. Sasa kwa nini walimu na polisi wanahangaika namna hii?” alihoji mtoa habari wetu.
AMANI LASAKA UKWELI
Baada ya kunyetishiwa ubuyu huo, mapaparazi wetu walizama mtaani ili kujiridhisha. Ilibidi mapaparazi wetu wamtafute Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mbezi Beach, Pantaleo Mushi ambaye alikiri kuwa, baadhi ya nyumba katika eneo hilo ni za wafanyakazi wa TRA.
“Ni kweli baadhi ya nyumba za mtaa wangu ni za watu wa TRA, lakini hayo mengine siyafahamu kabisa. Ila kama mnataka kujua zaidi, nendeni wenyewe. Maisha ya watu ni utaratibu wao wenyewe, wanavyoishi ni vile watakavyo,” alisema.
Amani: “Vipi lakini, kukiwa na vikao vya serikali za mtaa wanajitokeza?”
Mwenyekiti: “Wanafika…wanafika.”
Amani: “Mbona tunasikia wanatuma wawakilishi?”
Mwenyekiti: “Labda wanapokuwa na udhuru.”
land-rover-range-rov-8_1600x0wMfano wa mikoko wanayomiliki.
KIJANA NA AMANI
Baada ya kuzungumza na mwenyekiti huyo, juzi, saa 5:28 asubuhi, gazeti hili lilimpigia simu kijana huyo ambapo baada ya mwandishi kujitambulisha jina na chombo cha habari, alikata simu.
ILIVYOKUWA IKIJULIKANA
Baadhi ya watu waliozungumza na Amani kuhusu vigogo wa TRA kujenga majumba ya kifahari maeneo ya Mbezi Beach walisema kuwa, awali waliamini kwamba, nyumba za maeneo hayo nyingi ni za wafanyabiashara na Wazungu waliweka makazi yao nchini.
“Jamani mimi nilipokuja kugundua kwamba, waliojenga Beach wengi ni jamaa wa TRA, TRL (Shirika la Reli Tanzania) na TPA (Mamlaka ya Bandari Tanzania), nilishangaa sana, zamani nilijuwa ni wafanyabiashara wakubwa na Wazungu wanaoishi nchini,” alisema Hamud Hassan Lukwu, mkazi wa Mbezi.
Akizungumza na wakazi wa Ngarenaro jijini Arusha hivi karibuni akiwa njiani kuelekea kwenye Kambi ya Jeshi Monduli, JPM alisema kuwa, mpango wake wa kutumbua majipu viongozi wa serikali ambao wanatumia pesa za umma kwa manufaa binafsi utaendelea mpaka watakapokwisha wote.
mercedes-benz-cls-class-01TAKUKURU WATOA NENO
Akizungumza na wanahabari jijini Dar juzi, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru), Valentino Mlowola alitoa onyo kwa taasisi nyeti nchini, zikiwemo zinazohusika na matumizi ya fedha za umma kufuata sheria, taratibu na kanuni.
Mlowola alisema kumekuwepo na malalamiko mengi kwa wananchi kuwajulisha matendo ya rushwa na ufisadi yanayoendelea hapa nchini.
Alisema kutokana na hali ya wananchi kuona nia ya serikali ya awamu ya tano katika kushughulikia matatizo ya rushwa na ufisadi ametoa onyo kwa maofisa wa umma wanaofanya rushwa na ufisadi kuwa sehemu yao ya kazi na miradi ya kuwaingizia kipato kuacha mara moja.

Everything You Need to Know About the Zika Virus Outbreak


GILLIAN MOHNEY,Good Morning America