Nape ampongeza Diamond kutumbuiza Afcon

 amNapepongeza Diamond kutumbuiza Afcon

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (kushoto) akimkabidhi bendera ya Taifa, Diamond Platnumz katika hafla ya kumuaga iliyofanyika Dar es Salaam jana. Msanii huyo anakwenda Gabon kutumbuiza ufunguzi wa mashindano ya Afcon yatakayoanza keshokutwa. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice-Tanzania, Salum Salum na mchekeshaji Joti. (Picha na Cosmas Mlekani).
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amempongeza mwanamuziki wa Tanzania, Nassib Abdul ‘Diamond Platnumz’ kwa kupata nafasi ya kutumbuiza kwenye ufunguzi wa fainali za Mataifa ya Afrika, Afcon.

Michuano hiyo itakayofanyika Gabon inatarajiwa kuanza keshokutwa hadi Februari 5 mwaka huu ambapo mataifa 16 yatashiriki.

Nape akizungumza katika hafla ya kumkabidhi bendera ya taifa Diamond Dar es Salaam jana, alisema kitendo cha msanii huyo kwenda kutumbuiza katika ufunguzi huo ni heshima kubwa kwa Tanzania.

Alimtaka Diamond kwenda kuliwakilisha vizuri taifa licha ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, kutopata nafasi ya kushiriki fainali hizo.

No comments:

Post a Comment