Ni barua waliyoitia saini Maseneta 47 wakiionya Iran kuhusu mazungumzo ya kutafuta muafaka kuhusu utengenezaji wa bomu la nyuklia, wakionya kuwa maamuzi yoyote yatakayofanywa baina yao na Rais Barack Obama yatahitaji kupitia katika Seneti kabla na yanaweza kufutwa mara moja na Rais atakayemrithi aliyeko madarakani wakati huu.
Barua hii imeamsha hisia za kukerwa kwa baadhi ya viongozi wa chama cha Democratic huku baadhi ya Wabunge na Maseneta wa Republican wakikwepa kuweka saini zao kuidhinisha kilichoandikwa.
Baadhi ya wananchi wanaona hii ni dharau kwa Rais aliyeko madarakani, ingawaje wengine wanaona ni sawa na hatua sahihi.
No comments:
Post a Comment