Mkazi wa mjini Moshi akipita katikati eneo la
Kariakoo mji humo huku maduka yaki yamefungwa baada ya jumuiya ya wafanya
biashara Mkoa wa Kilimanjaro kuwamasishana kuyafunga wakipinga kutumia mashine
za EFD na kupandishwa kwa kodi ya mapato, mkoani humo jana. Picha na Dionis
Nyato
Wauzaji
na wamiliki wa maduka maeneo ya Mwanjelwa, Uhindini na Sido mkoani Mbeya jana
waliwalaumu viongozi wao kwa kuwashinikiza kuyafunga maduka bila kutoa sababu za
msingi na kuwasababishia hasara.
Wamesema
tabia ya kufunga maduka inawaathiri wao na wateja badala ya Serikali
inayolaumiwa.
Wakizungumza
kwa sharti la kutotajwa majina yao, wafanyabiashara hao walisema, viongozi wao
wanawalazimisha kuyafunga maduka na kwamba atakayefungua atalipishwa
Sh50,000.
No comments:
Post a Comment