Watanzania wa UK wagomea mradi mchafu wa kukaguliwa magari yao na kampuni binafsi.

Ndugu Mabloger na wana libeneke wakubwa

Mwanzo wa yote nataraji kuwa wote mko salama na mnaendelea vyema na uchapaji kazi kama kawaida.
Rejea kichwa cha habari hapo juu,tunaomba mtu peperushie hii habari ili wahusika wajue kitu wanachokifanya sio sawa na wasijaribu kutuburuza bila kutumia busara na kufuata sheria.
Ukitazama kwenye attachment utaona tangazo la TBS ambalo wanatangaza kuanzia tarehe 16/03/2015.Kuna kampuni binafsi inayomilikiwa na watanzania hapa Uk,ambao wanasemekana wameshinda zabuni ya kukagua magari yote yanayotarajiwa kuja Tanzania kwa gharama ya $200 kwa kila gari,hii ni uonevu na unyanyasaji kwa Watanzania wenzao,kwa sheria za UK kila gari inahitaji kukaguliwa na kutambulika kama ina hali ya kuendelea kuwa barabarani(MOT) ambayo kwa sasa iko digital,kupitia link za DVLA au VOSA gonga hapa.Hii MOT inafanywa na wataalamu walio bobea na wenye vifaa maalum,kwa magari madogo vituo viko kila mji na kwa maroli na mabasi kuna vituo maalumu,kwa magari madogo gharama yake ni £50 tu .

Tunasikitishwa kwa kitendo cha TBS kutangaza mzabuni huyu bila kufuata ushauri wa watanzania na wa kisheria ili zoezi zima liweze kukubalika na bila kuwaumiza watanzania.Iweje leo tulipie $200 kwa kampuni binafsi wakati kuna MOT yenye kiwango kuliko hii ya mtu binafsi na kwa pesa kubwa zaidi?Na hii kampuni inauwezo gani wa kukagua maroli na mabasi yenye kutaka kusafirishwa wakati ukaguzi wa hii unafanywa katika vituo maalum?Hii kampuni itakuwa na vituo vingapi ili kuweza kukidhi matakwa ya watanzania waishio UK.
Kwa kigezo kuwa kuna fake MOT,hiyo link juu ni sehemu ambayo kila mtu anaweza tizama uhalali wa MOT kwa kila gari iliyotoka UK.
Kifungu kipi cha sheria kinatumika kuweka kiwango hiki?,kulikuwa na kesi imefikia wapi hadi leo watujulishe kuwa kuna mzabuni na gharama hizi kubwa.Hii ni aina ya uongozi usio jali maslahi ya watanzania na wasio weza wapunguzia mzigo wenzao kisa matakwa yao binafsi ya kujitajirisha tu.Mfano mzuri ni kuwa mtu yuko North katika miji kama Leeds au Sheffield,ambako kuna vituo vya MOT lakini kwa utaratibu huu anapaswa kuleta gari yake London,Tulibury port kwenye ofisi hizi binafsi kisha atume gari yake.Wakati kuna vituo vya MOT kila mahali na kuna bandari North sio lazima kuleta gari London.Huu si uhungwa hata kidogo.
Watanzania wote walioko UK wanapinga utaratibu huu mpya wa kuhujumu watanzania na kuomba serikali na shirika lake la viwangi kusitisha zoezi hili mara moja na kutizama utaratibu mzuri wa kutumia MOT za serikali.

Kwa pamoja watanzania wa UK wameanza kuweka sahihi ya kuomba kusitishwa utaratibu huu gonga hapa kwenda kwenye petition.Tunaomba kuwajulisha wahusika hali hii haitaweza kukubalika kwa sasa wala baadae kwa kuwa huu ni mradi wa kunufahisisha watu wachache tu.Tunatanguliza shukrani kwa wana habari wote wenye kusambaza habari hii na kuomba wananchi wajiandikishe kupinga hali hii ya uonevu na unyanyasaji.

Ni sis wana
Diaspora UKTz

NB;
Link ya petition.
Ikiwa hapo juu haipatikani
http://www.change.org/p/tanzania-goverment-foregn-affiars-tanzania-bureau-of-standard-tbs-to-stop-to-use-serengeti-freight-in-uk-for-vehicle-inspection-before-shipping-to-tanzania

No comments:

Post a Comment