Treni mpya ya abiria yenye kufanya safari
zake kati ya Dar es Salaam na mikoa ya Kigoma na Mwanza, ikiwa kwenye kituo
kikuu cha reli (TRL), jijini Dar es Salaam leo Jumatano Aprili 1, 2015. Treni
hiyo iliyopewa jina "Deluxe Coach" imezindua safari yake ya kwanza leo Aprili
mosi, kuelekea Kigoma, ikiwa na mabehewa mapya yaliyoagizwa na serikali hivi
karibuni. Injini zilizokarabatiwa na wamalaysia, zimeonekama kama mpya na sasa
treni hiyo itakuwa ikisafiri kila Jumapili saa 2 usiku ikitumia masaa 30, ambayo
ni pungufu ya masaa 6 yanayotumiwa na treni ile ya kawaida. Kwa mujibu wa Meneja
Mkuu wa TRL, Kipallo Aman Kisamfu aliiambia K-VIS blogu kuwa treni hiyo
haitakuwa na vituo vingi na kutaja kuwa iking'oa nanga Dar es Salaam, kituo cha
kwanza ni Morogoro, na kufuatiwa na Kilosa. Baada ya hapo itasimama kwenye
stesheni ambazo ziko Wilayani na mikoani. Treni hiyo itakuwa na madaraja ya tatu
ambayo hutumiwa na "makabwela", daraja la pili kukaa, daraja la pili kulala,
daraja la kwanza na pia patakuwa na hoteli ya kisasa kabisa. treni hiyo mpya
inazo huduma za maji kwenye vyumba na vyoo. Meneja mkuu huyo wa TRL ametoa wito
kwa watumiaji, kwa kusema neno moja tu "Tukitunze"
Abiria wa kwanza wanaoelekea Kigoma,
wakifurahia uzuri wa mabehewa hayo
No comments:
Post a Comment