Basi la Majinjah baada ya kuangukiwa na lori
wilayani Mufindi, Iringa lilipokuwa likitokea Mbeya kwenda Dar es
Salaam.
Dar
es Salaam. Ajali za vyombo vya usafiri wa majini na barabarani huenda
zikaendelea kutokea nchini na kuchukua uhai wa watu wengi zaidi kila kukicha
kutokana Serikali kuwaadhibu madereva tu na kuwaacha maofisa waliohusika na
miundombinu mibovu na wanaoshindwa kukagua ipasavyo vyombo hivyo.
Kila
zikitokea ajali za barabarani, Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani
hukimbilia kuwakamata madereva na kuwafungulia mashtaka na wakati mwingine
wamiliki wa vyombo hivyo, lakini siyo maofisa waliosababisha barabara kujengwa
chini ya kiwango, nyembamba au kuacha mashimo bila kuyafukia wala maofisa
wanaoacha kukagua magari.
No comments:
Post a Comment