Nafikiri wote tumesikia na kusoma kwenye
mitandao mbali mbali kuhusu ndoa ya Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dr. Reginald
Mengi na former Bongo Flava Artist Jacqueline Ntuyabaliwe (K-Lynn). Ndoa hiyo
amabayo inasemekana kufungwa katika visiwa vya Mauritius na watu wachache sana
wameweza kuhudhuria tukio hilo; katika hao watu wachache inasemekana hakuna
mtoto wake hata mmoja (kutoka kwa ndoa yake na mke mkubwa) ambaye alikuwa hapo
kushuhudia tukio hilo. Pia vile vile hakuna ndugu wala jamaa wa karibu kabisa wa
Dr. Mengi ambaye alialikwa kushuhudia ndoa hiyo! Hili swala limenikumbusha kitu
ambacho kilishawahi tokea miaka ya huko nyuma ambacho kilipelekea Mr. Mengi
kuita waandishi wa habari na kukanusha tuhuma hizo.
Mwaka
2009 kuna picha zilitumwa mitandanaoni ambazo zilionyesha Dr. Mengi na mdada
aitwaye Lilian Kimaro ( wengi tuliziona) pamoja na watu wengine wakiwa kwenye
sherehe fulani. Mavazi yao na mazingira ya party yalikuwa yakiashiria watu hao
wawili na wengine walio kuwepo kwenye picha kuwa ilikuwa ni sherehe fulani
muhimu. Wajuzi wa habari wakitoa taharifa kwamba by then Mr. Mengi now ni "Dr.
Mengi" amefunga ndoa na mrembo huyo (Lilian Kimaro), kitu ambacho Dr. Mengi
alikuja akakanusha kwa kusema ni kuwa ni uzushi tuu wakutaka kumchafulia jina,
pia akahusisha jambo hilo na jitihada zake za kupinga ufisadi. Unaweza
kujikumbusha story hiyo kwa link hizi zifuatazo:-
Kusoma
zaidi bonyeza HAPA
No comments:
Post a Comment