Idadi
ya vifo vinavyotokana na joto kali nchini India vimepita zaidi watu 1,000 huku
hali ya joto ikikaribia nyuzi joto 50 katika baadhi ya maeneo.
Vingi
ya vifo vimetokea katika jimbo la kusini la Telangana pamoja na Andhra Pradesh,
ambapo watu 1,118 wamekufa tangu wiki iliyopita.
Ripoti
zinaeleza watu wengine 24 wamekufa kutokana na joto kali huko Bengali Magharibi
pamoja na Orissa. Hali ya joto hilo inatarajiwa kupungua katika siku chache
zijazo.
No comments:
Post a Comment