Mwenyekiti
wa Soko la Mchikichini-Ilala Jumanne Kongogo akizungumza na baadhi ya waandishi
wa habari waliofika katika Ofisi za Soko la Mchikichini-Ilala jijini Dar es
Salaam leo, kuhusiana na wafanyabiashara Walemavu kufunga barabara ambayo
inaruhusu magari kutoka na kuingia katika soko hilo, magari ambayo yanatoa
huduma katika soko hilo.
Katibu wa
soko la Mchikichini-Ilala jijini Dar es Salaaam John Andrew akionyesha takataka
zilivyo lundikana katika eneo la soko la Mchikichini-Ilala baada ya
wafanyabiashara kuziba njia inayoruhusu magari kuingia na kutoka nje ya soko
hilo, ambapo hata magari yanayochukua uchafu katika soko hilo yanashindwa
kufika.kuchukua uchafu huo.
Mlundikano
wa Takataka katika Soko la Mchikichini-Ilala jijini Dar es Salaaam ambazo
zimekuwa kero kwa wafanyabiashara wa eneo hilo.
Hili ni
eneo la kuegesha magari lakini wafanyabiashara wamegeuza kuwa sehemu ya kuuzia
bidhaa zao eneo katika Soko la Mchikichini-Ilala jijini Dar es Salaam. Picha
na Emmanuel Massaka.
No comments:
Post a Comment