Leo tunakutana na staa wa filamu na mwanamitindo Bongo, Neema Chande ambaye amejichimbia nchini India akifanya biashara pamoja na urembo. Mdada huyo alibanwa maswali 10 na Mwandishi Wetu Hamida Hassan. Kaulizwa nini na akajibu vipi? Fuatilia hapa chini…
Ijumaa: Hongera kwa kujifungua salama, hivi ni mama nani na unajisikiaje kuitwa mama?
Neema: Naitwa Mama Clara, najisikia amani sana kwani nilijikuta napata raha ambayo sijawahi kuipata.
Ijumaa: Kuna madai kuwa mtoto ni wa DJ wa Diamond, Rommy Jones, je kuna ukweli wowote?
Neema: Rommy tuliachana kitambo, baba wa mtoto ni mwanaume ambaye ndiye aliyeniposa, ndoa hivi karibuni.
Ijumaa: Mbali na uanamitindo unajishughulisha na fani gani nyingine huko India?
Neema: Huku nina biashara zangu kwani nina saluni ya kike pia nina sehemu ya kupika chakula, vyote vinaniingizia kipato.
Ijumaa: Una mtoto mmoja sasa, je unafikiria kuongeza mwingine?
Neema: Nafikiria kuongeza wa pili mara huyu atakapokua mkubwa.
Ijumaa: Ulishawahi kutoka na wanaume wangapi? Unawaambia nini wasichana wanaopenda kubadili wanaume?
Neema: Swali gumu hilo kulijibu, ila kwa wasichana wenzangu wanaopenda kurukaruka nawashauri watulie kwani hali ni mbaya.
Ijumaa: Pamoja na kuzaa bado unaendelea kuonekana mrembo, nini siri ya mafanikio yako?
Neema: Mume wangu ndiyo ananitunza na kunifanya nionekane mrembo licha ya kuzaa.
Ijumaa: Ukiwa na Baba Clara faragha unapenda kukaa pozi gani? Na mavazi gani unapendelea kuvaa?
Neema: Napenda kuvaa mavazi yanayonifanya nionekane sex, mapozi yangu ni yale yanayomfanya mpenzi atambue kuwa yuko na mimi.
Ijumaa: Chakula unachopenda kumpikia mwanaume wako ni kipi?
Neema: Mseto uwe na kuku au nyama, atajilamba mpaka basi.
Ijumaa: Ulishawahi kugombea mwanaume? Unawaambiaje wale ambao kila kukicha ni mabifu kisa wanaume?
Neema: Sijawahi kugombea mwanaume, sina historia hiyo ila nawaambia kuwa hiyo siyo dili, ukiona mwanaume amekuacha ujue siyo riziki yako.
Ijumaa: Unawaambiaje mashabiki wako uliowaacha kitambo Tanzania?
Neema: Kwanza najua wamenimis na wanajiuliza niko wapi, soon nitawajuza nilikuwa nafanya nini kwani ukimya mwingi una kishindo.
No comments:
Post a Comment