Watu wenye silaha washambulia hoteli Mali

Radisson Blu HotelImage captionTovuti ya hoteli hiyo inaieleza kama "hoteli ya kifahari"

Watu wenye silaha wameshambulia hoteli ya Radisson Blu katika mji mkuu wa Mali, Bamako, ripoti zinasema.

"Kuna dalili kwamba hili ni jaribio la kuwachukua watu mateka. Polisi wako hapo na wamezingira eneo hilo," duru za kiusalama zimeeleza shirika la habari la Reuters.

Milio ya risasi inasikika kutoka nje ya hoteli hiyo yenye vyumba 190, shirika la habari la AFP linasema.

Mwandishi wa BBC Afrique Abdourahmane Dia anasema hoteli hiyo, inayomilikiwa na Wamarekani, hutumiwa sana na raia wa kigeni wanaofanya kazi nchini Mali.

No comments:

Post a Comment