Mgomo wa mabasi Mwanza abiria wateseka saa 10 stendi

abiria wakisubiri usafiriabiria
Baadhi ya abiria wakisubiri usafiri bila mafanikio.
akizungumzakaimu mkurugenzi akizungumza na maderevakaimu mwenyekiti wa mkurugezi halimashauri ya wilaya ya Ilemela Juma Kasendeko
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela, Mwanza, Juma Kasendako akiongea na madereva wa mabasi.
mabasi stendimagari yakiwa yamepaki
Mabasi yakiwa yameegeshwa stendi.
mwenyekiti wa madereva kanda ya ziwa dede Hassan Petro akifafanua jambo katika stendi ya Igombe mwanza
Mwenyekiti wa madereva Kanda ya Ziwa, Dede Hassan Petro akifafanua jambo katika stendi ya Igombe, Mwanza leo.
Na Idd Mumba, Mwanza
LEO katika Jiji la Mwanza kumetokea mgomo wa magari ya kwenda Kata ya Igombe wilayani Ilemela kutokana na barabara waliyokuwa wanaitumia kutoka Mwanza mjini hadi Igombe kufungwa kwa ajili ya upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mwanza na badala yake kuelekezwa kutumia njia nyingine ambayo ni mbovu bila kupewa maelekezo yoyote na mamlaka husika kuhusu mabadiliko hayo pamoja na mabadiliko ya nauli kutokana na umbali kuwa mrefu kuliko ilivyokuwa awali.
Mgomo huo ambao umedumu takribani saa 10 bila gari yoyote kutoka wala kuingia mjini jambo ambalo limetoa adha kubwa kwa wasafiri wanaotumia barabara hiyo hadi mwenyekiti wa madereva kanda ya ziwa alipofuatilia suala hilo Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela ili kupata ufafanuzi zaidi kuhusu suala hilo.
Kwa upande wake. Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela, Juma kasendako alipotoa maelezo ya kuwa suala hilo litapatiwa ufumbuzi wa kina ifikapo kesho Jumatano hivyo wamiliki na madereva wametakiwa kuendelea na kutoa huduma zao kama kawaida mpaka mamlaka husika zitakavyokaa na kujadiliana kuhusu bei elekezi kutokana na mabadiliko ya barabara hiyo.

No comments:

Post a Comment