Kitilya na wenzake wazidi kusota Mahakama ya Rufaa Dar

2Sioi Sumari akiwa na askari wa magereza.
3Shose Sinare naye akiongozana na askari magereza kuelekea kwenye gari lililompeleka rumande.
4Baadhi ya mawakili na wananchi wakitoka mahakamani.
LEO katika Mahakama ya Rufaa Tanzania, jijini Dar es Salaam Kamishna Mkuu mstaafu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya na wenzake  waliokuwa wafanyakazi wa Benki ya Stanbic Tanzania, Sioi Sumari na Shose Sinare walifikishwa mahakamani hapo kusikiliza rufaa iliyokatwa na upande wa Jamhuri.
Jamhuri imekata rufaa kupinga kufutwa shitaka namba 8 linalowakabili wote kwa pamoja la utakatishaji fedha linalowakabili. Hata hivyo, mahakama hiyo itapanga tarehe ya kusikilizwa shauri hilo siku itakayotangazwa.
Washitakiwa hao wanakabiliwa na shitaka la kula njama na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kinyume na sheria na walifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Aprili Mosi, mwaka huu wakikabiliwa na mashtaka nane likiwamo la utakatishaji wa dola za Kimarekani milioni sita ambazo ni sawa na zaidi ya Sh bilioni 12.
Mashtaka yao yanatokana na tuhuma za ufisadi ulioipotezea serikali zaidi ya Sh. trilioni 1.3 katika kipindi cha kati ya mwaka 2012 na 2013 za uuzaji wa hati fungani.
PICHA NA HABARI NA DENIS MTIMA

No comments:

Post a Comment