Sehemu ya mashabiki wakiwa ndani ya Dar Live.
Isha Mashauzi akipagawisha mashabiki.
Snura Mushi ‘Mamaa Chura’ (katikati) akitoa burudani.
Man Fongo akirindimisha burudani ya Singeli.
Inspekta Haroun akiwanogesha mashabiki baada ya kupanda jukwaani na kufanya yake.
Mwimbaji wa Mashauzi Classic, Saida Makongo, akiwa kazini.
Huyu ni Hashim Said wa Mashauzi Classic.
WAPENZI wa burudani usiku wa kuamkia leo walipata uhondo wa aina yake ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live wakati wakali wa kutoa burudani, Snura Mushi maarufu kama Mamaa Chura, Mashauzi Classic Modern Taarab, Man Fongo na wakali wengine walipoonyesha makali yao.
Katika tamasha hilo lililohudhuriwa umati wa mashabiki ilikuwa ni mwendo wa ‘kukata kilaji’ na kuserebuka mwanzo-mwisho.
Burudani ya muziki ukumbini hapo ilifunguliwa na Mashauzi Classic, chini ya Isha Mashauzi, ambao waliachia vibao vyao vipya na vinavyoendelea kutamba na kuwanogesha mashabiki.
Burudani ya muziki ukumbini hapo ilifunguliwa na Mashauzi Classic, chini ya Isha Mashauzi, ambao waliachia vibao vyao vipya na vinavyoendelea kutamba na kuwanogesha mashabiki.
Baada ya Isha na kundi lake kukamua vya kutosha, Mamaa Chura na wanenguaji wake walirukia jukwaa kwa staili zao za kudatisha lakini zikiwa na ustaarabu wa kimaadili na kunogesha mambo ukumbini.
Wapenzi wa burudani wakati wakiendelea kupiga mayowe ya kumshangilia ‘Chura’ mkali wa Singeli kutoka pande za Uswazi, Man Fongo aliingia na kubadilisha mandhari kwa staili yake ya singeli.
Baada ya Man Fongo kuwapeleka puta mashabiki katika hali ya ‘sapraiz’, Inspekta Haroun ‘Babu’ na JB ‘Mkuu wa Maadui’ nao kila mmoja alipanda jukwaani kwa muda wake na kufanya makamuzi na kushangiliwa na mashabiki.
PICHA/ STORI: RICHARD BUKOS / GPL
No comments:
Post a Comment