By Malisa GJ
Baada ya timua timua ya wanafunzi walioko vyuoni imeonekana kuna watu wanajadili vitu wasivyovijua vizuri. Watu wengi wanaonekana kuchanganya kati ya wanafunzi waliotimuliwa UDOM na wale waliotimuliwa vyuo vingine kwa kukosa sifa. Ni vizuri wakati wa kujadili tukaelewa tunajadili kundi gani kati ya haya mawili.
#KUNDI_LA_KWANZA ni wale waliopata division one hadi three na wakapata alama "A" au "B" kwenye masomo ya Sayansi (Physics, Maths, Chemistry, Biology). Hawa walidahiliwa chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) kwa program maalumu ya miaka mitatu ya kupata diploma ya ualimu wa sekondari.
Utaratibu huu haukuanzishwa na wanafunzi hawa. Ulianzishwa na Rais JK na kupigiwa vigelegele na wafuasi wote wa CCM. Leo JPM anaona ni utaratibu wa hovyo na anawaadhibu wanafunzi kwa kuwafukuza. Cha ajabu wafuasi walewale waliomshangilia JK akianzisha mfumo huu ndio haohao wanaomshangilia JPM akiufuta. Huu ni uzwazwa wa shahaha ya juu kabisa ya uzamivu uliobobea (PhD with gigantic Experiece).
Kwanini tunawahukumu watoto wasio na hatia? Yawezekana tunahitaji marekebisho ktk mfumo wa elimu lakini si kwa style hii. Nadhani kama JPM angekua na busara angesubiri watoto hawa wamalize kisha ndo aufute huu mfumo. Lakini kuufuta sasa hivi wakati ameshawapotezea miaka mitatu ni ukatili. Wanafunzi hawa wangeendelea form five (sifa wanazo) kwa sasa wangekua first year chuo kikuu. Kwahiyo wanafunzi waliotimuliwa UDOM hawajafeli kama inavyoenezwa.
Na kama mfumo huu ulikua haufai kwanini vijana wa CCM mlimshangilia JK alipokua anauanzisha? Si mngemwambia tu wazi kuwa Mzee hii si sawa. But mlipiga makofi kumshangilia halafu leo amekuja mtu mwingine ameufuta
No comments:
Post a Comment