Baada ya kuachika… Mariam wa BSS awa chapombe!

Mariam wa BSS (2)Mariam Mohammed Uwesu ‘Mariam wa BSS’ na Emeraa.
NA Richard Bukos, RISASI mchanganyiko
DAR ES SALAAM: Mshindi wa Shindano la Bongo Star Search (BSS) 2010, Mariam Mohammed Uwesu ‘Mariam wa BSS’ hivi sasa amekuwa mtu wa kupata kinywaji kingi ‘cha pombe’, ikiwa ni mwezi mmoja tu baada ya kupewa talaka na mumewe.
Mariam aliolewa mwaka 2014 na mumewe Hassan Hamis ‘Soda ya Kopo’ kabla ya kuachika baada ya kupishana ‘mahesabu’ ambapo mwanaume huyo alimkabidhi talaka na kila mmoja  akashika hamsini zake.
Mariam wa BSS (1)Mariam wa BSS akibugia pombe.
Juzikati mrembo huyo alinaswa katika Ukumbi wa Mango Garden jijini Dar akiwa anakula ulabu mwingi huku akijirusha kimahaba na njemba aliyefahamika kwa jina la Emeraa wakipeana kampani ya wapendanao.
Wawili hao walionekana kuwa ‘ziro distance’ huku wakati mwingine wakinyweshana vinywaji hali iliyoanza kuzua minong’ono kwa wambeya waliokuwa wakiwapiga chabo ukumbini hapo.
“Mh! Huyu si aliolewa huyu? Mara hii kishaachika na kunasa mtu mwingine? Kweli hawa mastaa ni noma aisee,” alisikika mpenda ubuyu mmoja.
Mariam na ‘baby’ wake huyo mpya hawakuonekana kuwajali wambeya hao, kwani waliendelea na mambo yao na ndiyo kwanza walizidisha vituko kama vile walikuwa wakimuumiza roho mtu fulani aliyekuwa ukumbini hapo.
Kama hiyo haitoshi, wawili hao walijitosa sehemu ya kuchezea ambapo mambo yalizidi kunoga kwa kuanza kucheza kwa staili za kichokozi huku wakilegezeana macho.
Baada ya wawili hao kurudi vitini kupunga upepo kidogo, paparazi wetu alizungumza na Mariam ambaye alisema ameamua kujirusha kihasira baada ya kuachana na mumewe.
“Nishindwe kujirusha kuogopa nini, yeye si kanipa talaka, acha nijirushe, talaka yangu amenipa tangu mwezi uliopita.
“Kwanza alinibana sana mpaka nikawa nashindwa kujiachia kama hivi, ndiyo maana ukawa hunioni sehemu kama hizi, huyu ndiyo niko naye kwa sasa,” alisema Mariam.
Wakati Mariam wa BSS akiweka hayo hadharani, Emeraa ambaye ni mpiga gitaa wa Jahazi Modern Taarab alimwambia paparazi wetu kuwa wana mpango wa kufunga ndoa.
“We kaa mkao wa kula, ndoa yangu na Mariam inakuja,” alisema Emeraa.

No comments:

Post a Comment