CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) MAAZIMIO YA KIKAO CHA KAMATI KUU ILIYOFANYIKA HOTELI YA BAHARI
BEACH LEDGER PLAZA, 23-26 JULAI, 2016
1.0 UTANGULIZI
Kamati Kuu ya dharura ya Chama iliketi kuanzia tarehe 23-26 Julai, 2016 Jijini Dar Es Salaam na ilikuwa na ajenda moja mahsusi ambayo ni kujadili hali ya siasa na uchumi wa Taifa tangu serikali ya awamu ya tano ilipoingia madarakani mwezi Novemba, 2015.
Mwenendo wa serikali hii ya CCM ya awamu ya tano, chini ya Rais John Magufuli, ni dhahiri kuwa umeamua kuiweka demokrasia kizuizini na kuleta utawala wa Kidikteta katika nchi yetu.
2.3 Kudhibiti Wabunge wa Upinzani Bungeni: Serikali imejificha nyuma ya kiti cha Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson Mwansasu (Mb) ili kuwadhibiti Wabunge wa Upinzani Bungeni kwa lengo la kuwanyamazisha wasiikosoe Serikali.
Ikumbukwe kwamba Dkt. Tulia akiwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali alikuwa ni mtumishi wa umma asiyepaswa kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa; lakini ghafla anaonekana akigombea nafasi ya Naibu Spika kupitia CCM. Hivyo yupo Naibu Spika ambaye ni mteule wa Rais. Swali: Anawajibika kwa nani kati ya Bunge na Rais?
Kuingilia Mhimili wa Mahakama: Serikali ya CCM kupitia Rais, kwa nyakati tofauti imeonekana kujaribu kuingilia uhuru wa Mahakama jambo ambalo ni hatari kwa utoaji wa haki nchini. Katika hotuba yake, wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria duniani Rais alinukuliwa akisema kwamba Mahakama iwahukumu harakaharaka watu waliokwepa kodi halafu atatumia asilimia fulani ya fedha ambazo zitakuwa zimepatikana kutokana na faini za wale walioshindwa kesi kuwapa Mahakama.Muswada wa Sheria ya Haki ya kupata habari –Serikali imepeleka Bungeni Muswada wa Sheria ya Haki ya kupata habari. Sheria hii imeweka adhabu kubwa sana kwa waandishi kama vile kifungo cha miaka 15 na kisichozidi miaka 20 kwa mujibu wa kifungu cha 6(6)
Kupuuza Utawala wa Sheria: Tarehe 24 Juni, 2016 wakati wa uzinduzi wa siku ya usalama wa raia, Rais Magufuli alinukuliwa akiwaruhusu polisi kuwaua majambazi bila kuwafikisha mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake. Aidha aliuagiza uongozi wa Jeshi la Polisi kuwapandisha vyeo watakaowauwa majambazi.Serikali hii inatishia ukuaji wa uchumi
Tangu serikali ilipoingia madarakani hali ya ukuaji wa uchumi na hata uwekezaji wa mitaji imekuwa ikiporomoka kwa kasi kubwa sana nchini mwetu na hata baadhi ya wawekezaji wanaondoa mitaji yao kutokana na serikali hii kukosa mwelekeo unaoeleweka wa Kiuchumi.
Serikali za mitaa kunyanganywa mapato na serikali kuu.
Baada ya uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 tulifanikiwa kushinda maeneo ya Majiji ya DSM, Mbeya,Arusha na Miji mikubwa ya Iringa, Moshi,Bukoba,Babati,Tunduma na mingineyo ya maeneo ya mijini ambayo kwa kiasi kikubwa wanategemea sana kuendesha Halimashauri hizo kwa kutumia kodi ya Majengo Kodi ya Majengo inachangia kati ya 30% hadi 60% ya mapato ya ndani ya Mamlaka za Miji.

- MATUKIO MAHSUSI YA UKANDAMIZAJI WA HAKI NA DEMOKRASIA
- Kupiga Marufuku Mikutano ya Vyama vya Siasa: Serikali kupitia Waziri Mkuu na hatimaye Rais na jeshi la Polisi walitangaza kwa nyakati tofauti kwamba ni marufuku kwa vyama vya siasa kufanya mikutano ya kisiasa mpaka mwaka 2020 ili kuipa Serikali nafasi ya kufanya kazi. Huu ni uvunjaji wa Ibara ya 20 (1) ya Katiba. Aidha, katazo la mikutano ya siasa linakiuka Sheria namba 5 ya Vyama vya siasa ya mwaka 1992 kifungu cha 11 ambayo imetoa haki kwa vyama vya siasa kufanya kazi ya siasa.
2.3 Kudhibiti Wabunge wa Upinzani Bungeni: Serikali imejificha nyuma ya kiti cha Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson Mwansasu (Mb) ili kuwadhibiti Wabunge wa Upinzani Bungeni kwa lengo la kuwanyamazisha wasiikosoe Serikali.
Ikumbukwe kwamba Dkt. Tulia akiwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali alikuwa ni mtumishi wa umma asiyepaswa kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa; lakini ghafla anaonekana akigombea nafasi ya Naibu Spika kupitia CCM. Hivyo yupo Naibu Spika ambaye ni mteule wa Rais. Swali: Anawajibika kwa nani kati ya Bunge na Rais?
Kuingilia Mhimili wa Mahakama: Serikali ya CCM kupitia Rais, kwa nyakati tofauti imeonekana kujaribu kuingilia uhuru wa Mahakama jambo ambalo ni hatari kwa utoaji wa haki nchini. Katika hotuba yake, wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria duniani Rais alinukuliwa akisema kwamba Mahakama iwahukumu harakaharaka watu waliokwepa kodi halafu atatumia asilimia fulani ya fedha ambazo zitakuwa zimepatikana kutokana na faini za wale walioshindwa kesi kuwapa Mahakama.Muswada wa Sheria ya Haki ya kupata habari –Serikali imepeleka Bungeni Muswada wa Sheria ya Haki ya kupata habari. Sheria hii imeweka adhabu kubwa sana kwa waandishi kama vile kifungo cha miaka 15 na kisichozidi miaka 20 kwa mujibu wa kifungu cha 6(6)
Kupuuza Utawala wa Sheria: Tarehe 24 Juni, 2016 wakati wa uzinduzi wa siku ya usalama wa raia, Rais Magufuli alinukuliwa akiwaruhusu polisi kuwaua majambazi bila kuwafikisha mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake. Aidha aliuagiza uongozi wa Jeshi la Polisi kuwapandisha vyeo watakaowauwa majambazi.Serikali hii inatishia ukuaji wa uchumi
Tangu serikali ilipoingia madarakani hali ya ukuaji wa uchumi na hata uwekezaji wa mitaji imekuwa ikiporomoka kwa kasi kubwa sana nchini mwetu na hata baadhi ya wawekezaji wanaondoa mitaji yao kutokana na serikali hii kukosa mwelekeo unaoeleweka wa Kiuchumi.
Serikali za mitaa kunyanganywa mapato na serikali kuu.
Baada ya uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 tulifanikiwa kushinda maeneo ya Majiji ya DSM, Mbeya,Arusha na Miji mikubwa ya Iringa, Moshi,Bukoba,Babati,Tunduma na mingineyo ya maeneo ya mijini ambayo kwa kiasi kikubwa wanategemea sana kuendesha Halimashauri hizo kwa kutumia kodi ya Majengo Kodi ya Majengo inachangia kati ya 30% hadi 60% ya mapato ya ndani ya Mamlaka za Miji.
No comments:
Post a Comment