Ijumaa Wikienda lamkamatisha Mchina kwa Waziri!

mgodini (4)-001Mchina akimpiga Mtanzania huyo.
Stori: Mwandishi wetu , Risasi Jumamosi
GEITA: Kimenuka! Katika gazeti damu moja na hili la Ijumaa Wikienda toleo la Jumatatu iliyopita, ukurasa wa mbele kulikuwa na habari yenye kichwa; RAIS MAGUFULI; HUU NDIYO UNYAMA ALIOUFANYA MCHINA BILA KUFANYWA CHOCHOTE, ishu ilimfikia Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba na amekinukisha.
Katika habari hiyo, Mchina mmoja alitajwa kumtesa Mtanzania ambaye hakujulikana jina mara moja kwa kumpa kipigo kwa madai kuwa, aliiba madini kwenye Mgodi wa Nyamhuna uliopo Katoro mkoani hapa.
mgodini (2)Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba akikagua majeraha ya kijana aliyepigwa na Mchina huyo.
WIKIENDA KWA WAZIRI
Sasa, baada ya gazeti hilo kutoka, waziri Nchemba alilisoma gazeti hilo pendwa na kuamua kuchukua hatua baada ya kutoamini kuhusu ukatili huo na hivyo kwenda eneo la tukio kujionea mwenyewe.
WAZIRI MGUU NA NJIA
Jumatano iliyopita, waziri huyo alifunga safari hadi  kwenye mgodi huo kwa ziara ya kikazi lakini kubwa ikiwa ni kufuatia taarifa za mateso ya kijana huyo kutoka kwa raia wa China ambaye ni mmoja wa wamiliki wa mgodi.
mgodini (1)1Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba akiwa katika Gereza la Wilaya ya Geita.
KWANZA BAADA YA KUFIKA
Awali, waziri Nchemba alijiridhisha kwamba, kulikuwepo na tukio hilo la Mbongo huyo kuteswa na jamaa huyo wa Kichina kwa kumpa kipigo kilichomsababishia kupoteza fahamu.
WAZIRI ALIJUAJE?
Waziri Nchemba alilazimika kutinga mwenyewe ndani ya Gereza la Geita alikoshikiliwa kijana huyo ikidaiwa kwamba, alishitakiwa na mwajiri wake kwa kosa la wizi.
Katika mahojiano na uongozi wa gereza hilo,  Waziri Nchemba alibaini kuwa, kijana huyo ndiye anayeonekana kwenye picha iliyosambaa mtandaoni kwa uthibitisho wa makovu yaliyopo mwilini mwake na mavazi aliyovaa siku anateswa na wakati yupo gerezani hapo.
WAZIRI, KIJANA HADI MGODINI
Katika hali iliyoonesha kuwa, Waziri Nchemba ameamua kuwapigania Watanzania, alimchukua kijana huyo na kwenda naye mgodini kwa ajili ya kuwatambua waliomfanyia vitendo hivyo vya kinyama.
mgodini (5)Wachina wakiwa wamepangwa kwenye msitari ili aliyempigwa aweze kumtambua aliyemshushia kipigo hicho.
WAPO WABONGO
Katika zoezi hilo, kijana huyo aliwabaini Watanzania watano ambao ni walinzi wa mgodi huo na Mchina mmoja kwamba ndiyo walioshirikiana kumpiga hadi kumjeruhi.
KIBAO CHAGEUKA
Kufuatia zoezi hilo la utambuzi, Nchemba aliagiza wahusika hao wakamatwe mara moja kwa hatua zaidi za kisheria.
mgodini (6)Watuhumiwa mbaroni
MUHIMU KULIJUA HILI
Hata hivyo, tukio la Mbongo huyo kuteswa si lile la kibarua mwingine wa mgodi huo aliyejulikana kwa jina moja la Elisha, ambaye wiki iliyopita alidaiwa kuanguka kisha kupoteza maisha akikimbizwa Hospitali ya Wilaya ya Geita kwa matibabu ambapo kwenye mitandao ya kijamii, ilitumika picha ya kijana aliyeteswa kuwa ndiye Elisha kabla ya kufariki dunia.
mgodini (7)WIKIENDA LASHANGAZWA NA HILI
Kuhusu tukio la Mbongo huyo kuteswa, katika toleo la Wikienda, Jumatatu iliyopita, lilizungumza na msaidizi wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Geita ambaye alikataa kutaja jina, yeye alisema kijana huyo kweli aliteswa lakini alipaochiwa alirudi kwao, Bariadi, Shinyanga.
Alisema jeshi la polisi halikuchukua hatua yoyote baada ya mtendewa kutoripoti popote malalamiko ya kuteswa kwake.
mgodini (1)Mchina anayetuhumiwa kumpiga Mtanzania akiwa na watuhumiwa wenzake kwenye karandinga la polisi.
GLOBAL YAPONGEZWA
Baadhi ya wasomaji wa magazeti ya Global Publishers wameipongeza kampuni hiyo wakidai kuwa, imekuwa ikiandika habari kwa kuchimba sana na nyingi zimekuwa zikiwatatulia matatizo wananchi.
“Mimi nilisoma ile habari ya kwenye Ijumaa Wikienda, nikasikitika sana. Sasa nilipoona Waziri Nchemba amekwenda, nikajua amesoma gazeti. Kwa kweli nawapongeza sana Global kwa kufichua maovu,” alisema Mwadamu Hassan, mkazi wa mjini Geita.

No comments:

Post a Comment