Jacqueline Wolper alivyohamia CCM hivi kaibuni.
WAANDISHI WETU, IJUMAA
MSANII nyota wa fi lamu Bongo, Jacqueline Wolper hivi karibuni anadaiwa kuongea mbele ya Rais Dk John Magufuli akiwa bwii wakati alipopewa nafasi ya kuzungumza na wana-CCM mjini Dodoma baada ya kutangaza kujitoa Chadema.
Wolper alikuwa miongoni mwa wasanii walioalikwa kwenye mkutano mkuu wa CCM uliokwenda sambamba na Magufuli kukabidhiwa uenyekiti wa chama hicho kutoka kwa Rais Mstaafu Jakaya Kikwete.
Aliposimama mbele ya kipaza sauti katika umati wa wana CCM uliofurika katika mojawapo ya kumbi zilizomo ndani ya Dodoma International Convention Centre, Wolper alionekana kuwa aliyechangamka huku akiongea maneno yaliyoashiria kuwa ‘ameonja’ kidogo.
Katika ‘spichi’ yake, Wolper alionekana kumfagilia Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akisema anampenda sana, ambapo wakati akiendelea kurudiarudia maneno hayo, minong’ono ilianza ukumbini hapo huku baadhi ya wasanii wenzake wakiinama chini kwa kuona ‘soo’.
“Yaani wengi waliokuwa pale ukumbini waliona Wolper alikuwa kanywa pombe kwa jinsi alivyokuwa anaongea, wapo waliokuwa wanacheka na wengine kuinamisha vichwa vyao,” alisema mmoja wa wasanii aliyekuwa ukumbini hapo aliyeomba hifadhi ya jina lake.
Kufuatia madai hayo, Ijumaa lilimtafuta kiongozi wa Bongo Muvi aliyekuwa kwenye msafara huo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ ambapo alipopatikana alisema: “Ninachojua Wolper hakutakiwa kuongea sana pale na ndiyo maana hakuchukua muda mrefu ila hayo madai kuwa alipanda jukwaani akiwa amelewa, siwezi kuyazungumzia kwa kuwa sina ushahidi na najua hawezi kufanya hivyo.”
Naye Wolper alipopatikana kupitia simu yake ya mkononi, alisema anashangazwa na madai hayo kwa kuwa siku hiyo alikuwa katika dozi ya siku tatu, lakini pia asingediriki kwenda kuongea mbele ya viongozi wa chama akiwa amelewa.
“Watu wanaongea sana, kwanza nilikuwa niko kwenye dozi, hivyo sikuwa na fursa ya kunywa lakini hata kama ningekuwa sipo kwenye dozi, nisingediriki kwenda pale nikiwa nimekunywa pombe.
“Watu hawajui tu, ila kiukweli kuongea mbele za watu wengi inahitaji ujasiri na ndiyo maana huenda ongea yangu iliwafanya watu wanifi kirie tofauti,” alisema Wolper.
No comments:
Post a Comment