STORI KAMILI KUHUSU VITA YA POLISI NA MAJAMBAZI VIKINDU

Askari 80 wa Kikosi cha Kuzuia Fujo wakijiandaa kuondoka katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam jana, kuelekea kwenye mapori ya wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani kusaka majambazi na wahalifu. (Picha na Yusuf Badi).
SIKU moja baada ya majibizano ya risasi kati ya askari na watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi katika eneo la Vikindu wilaya ya Mkuranga katika mkoa wa Pwani, Jeshi la Polisi limetuma kikosi cha askari zaidi ya 80 kwenye operesheni maalumu katika maeneo ya Vikindu, Mkuranga na jirani kuwasaka majambazi.

Katika mapambano hayo yaliyodumu kwa saa saba katika Mtaa wa Vikindu Mashariki, Mkuranga, askari mmoja alipoteza maisha.

Akizungumzia operesheni inayoendelea ya kupambana na uhalifu katika maeneo hayo, Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro alisema operesheni hiyo ilianza tangu Alhamisi baada ya mauaji ya askari wanne waliokuwa wakilinda katika benki ya CRDB iliyopo Mbande katika Manispaa ya Temeke.

No comments:

Post a Comment