Kimbunga vyeti feki chazoa vigogo kibao
imbunga vyeti feki chazoa vigogo
kibao
HATIMAYE ile kazi ya kuhakiki vyeti halisi vya elimu
na taaluma za watumishi wa wizara na taasisi
mbalimbali za umma imeanza kuibua kilio cha aina
yake baada ya kubainika uwapo wa watumishi
kibao waliojipatia ajira kiujanja-ujanja kwa
kutumia vyeti bandia.
Na sasa, matokeo ya kimbunga cha uhakiki huo yameibua pigo la aina yake
lililoanza kuwakumba watumishi hao, wakiwamo vigogo wanaoshikilia nafasi
mbalimbali za juu katika taasisi na idara mbalimbali za Serikali.
Taarifa ambazo Nipashe ilizipata wiki hii kupitia vyanzo vyake na kisha
kuthibitishwa jana na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Menejimeti ya Utumishi wa
Umma, Dk. Laurean Ndumbaro, ni kwamba tayari kuna orodha ya watumishi
waliobainika kupata ajira wakitumia vyeti bandia na kwamba uchunguzi zaidi
unaendelea, huku hatua za kisheria na kinidhamu ziko mbioni kuchukuliwa
dhidi ya watuhumiwa wote wa udanganyifu huo.
Katika uchunguzi wake, Nipashe ilibaini kuwa baadhi ya watumishi hao
wakiwamo vigogo wanaojijua kuwa vyeti vyao vya kielimu vina utata, tayari
wameanza kujiondoa wenyewe kinyemela kwa kuacha kazi ghafla wakihofia
hatua za kisheria dhidi yao.
04
SEP
2016
9/5/2016 Kimbunga vyeti feki chazoa vigogo kibao
http://www.ippmedia.com/sw/habari/kimbunga-vyeti-feki-chazoa-vigogo-kibao 2/5
Operesheni kabambe ya kuhakiki uhalisia wa vyeti vya watumishi wote wa umma wakiwamo
vigogo katika taasisimbalimbali ilishika kasi tangua kuingia madarakani kwa Serikali ya
awamu ya tano chini ya Rais Magufuli, lengo mojawapo likiwa ni kuongeza ufanisi katika
kazi ya kuwatumikia Watanzania na pia kutoa fursa za ajira kwa wataalamu wa fani husika
katika kila nafasi na siyo “wataalamu bandia”.
“Huu uhakiki umeleta balaa… kuna watumishi hawana amani wakihofia hatima yao kwa
sababu wamekuwa wakitumia vyeti bandia kwa miaka mingi na badhi wanashikilia nafasi za
juu zenye mishahara na marupurupu makubwa,” chanzo kimoja kiliiambia Nipashe na
kuongeza:
“Hata hivyo, baadhi wamejua kuwa wako hatarini kuumbuka na kuchukuliwa hatua kali za
kisheria kutokana na kosa la kufoji (kughushi), na hivyo wameacha kazi wenyewe na
wengine wengi wa aina hiyo wanaachia ngazi kimyakimya.”
PANGA KUTEMBEA NCHI NZIMA
Baada ya kupata taarifa za kuwapo kwa vigogo na watumishi wengine kibao walioanza
kupatwa na kimbunga cha matokeo ya uhakiki wa vyeti, ndipo Nipashe ilipohitaji ufafanuzi
kutoka kwa Dk. Ndumbaro, ambaye alikiri kuwapo kwa watumishi wengi waliobainika kuwa
na vyeti bandia na kwamba baadhi yao wameanza kujiondoa wenyewe.
Kwa mujibu wa Dk. Ndumbaro, uchunguzi zaidi kuhusiana na watumishi na maafisa wa juu
wa serikali walioingia kwenye mfumo wa ajira bado unaendelea nchini kote na kwamba,
hakuna atakayesalimika ikiwa atakutwa na hatia hiyo.
Katibu Mkuu huyo alisema tayari wizara yake ina taarifa za kuacha kazi kwa baadhi ya
watumishi wakihofia kuchukuliwa hatua kwa kujijua kuwa wana vyeti bandia, lakini hadi
sasa wapo wengine wengi wanaoendelea na kazi huku wakisubiria kujua hatima yao kwa
kuwa uchunguzi kuhusiana na jambo hilo bado unaendelea.
“Zipo taarifa za watu kuacha kazi na wengine bado wanasubiria kujua hatima yao kwa
sababu uchunguzi unaendelea… kwa sasa ni vigumu kujua ni wangapi walioacha kazi kwa
kuwa tunaendelea na uhakiki wetu,” alisema.
Aidha, akizungumza na Nipashe jana, afisa mmoja msaidizi wa Dk. Ndumbaro aliiambia
Nipasahe kuwa idadi halisi ya watumishi walioacha kazi katika kipindi hiki cha uchunguzi wa
vyeti itakuwa tayari wiki inayoanzia kesho. Dk. Ndumbaro ndiye aliyemtambulisha afisa
huyo kwa Nipashe.
ILIVYOKUWA
Serikali ilianza kuweka wazi mikakati yake ya kuwabaini watumishi wenye vyeti bandia hivi
karibuni, ikitangaza pia kuanza rasmi kwa kampeni ya kuwashughulikia na kuwaondoa
katika utumishi wa umma watumishi wote walioajiriwa kwa vyeti visivyo na sifa.
Iliwataka watumishi hao waanze kujitathmini na kuanza kujiondoa wenyewe kazini kabla ya
kubainika kwani watafukuzwa kazi na kufikishwa mahakamani kwa makosa ya kugushi.
9/5/2016 Kimbunga vyeti feki chazoa vigogo kibao
http://www.ippmedia.com/sw/habari/kimbunga-vyeti-feki-chazoa-vigogo-kibao 3/5
Akizungumza bungeni mjini Dodoma wakati wa majumuisho ya Makadirio ya Mapato na
Matumizi ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2016/2017, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako alisema serikali imedhamiria kuboresha kiwango cha elimu
nchini na kwamba, hatua mojawapo inayochukuliwa ni kukagua uhalali wa vyeti vyote vya
elimu kwa watumishi wa umma katika sekta ya elimu na sekta nyinginezo.
Tamko la Waziri Ndalichako lilizua hofu, hasa kwa watumishi walioingia kwenye mfumo wa
ajira za serikali kupitia ‘vimemo’ kutoka kwa wakubwa huku wakiwa hawana sifa stahiki za
kufanya kazi walizopewa.
Baada ya kutangazwa kwa oparesheni hiyo, matangazo ya kupotea kwa vyeti vya elimu
katika vyombo mbalimbali vya habari yaliongezeka maradufu huku.
OPERESHENI YAGUSA KILA KONA
Hadi sasa, idara na taasisi mbalimbali za umma nchini kote zimeshafanya uhakiki kabambe
wa vyeti vya kielimu na kitaaluma kwa watumishi wao, baadhi zikiwa ni halmashauri za
Wilaya, Mamlaka ya Bandari (TPA), Mamlaka ya Mapato (TRA) na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi
ya Jamii (NSSF).
Kwa mfano, katika waraka mmojawapo wa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Prof. Godius
Kahyarara kwenda kwa wakurugenzi wengine, mameneja wa mikoa wa mfuko huo, maafisa
wa wilaya na wafanyakazi wote, na ambao ulisambazwa kwenye mitandao mbalimbali ya
kijamii ukionyesha kuwa na kumbukumbu namba NSSF/HQ/C/03/7Vol.II/120,
ilikumbushwa kwamba kwa kuzingatia maelekezo ya awali kupitia waraka wa Juni 13, kila
mmoja wao alitakiwa kuwasilisha nakala za vyeti vyake halisi vya elimu na fani walizosomea
kufikia Juni 24, 2016. Na kwamba, yeyote asiyefanya hivyo asingelipwa tena mshahara
kuanzia wa mwezi Juni mwaka huu hadi hapo atakapotimiza sharti hilo la kuwasilisha vyeti.
Waraka mwingine mmojawapo kati ya nyingi zilizosambaa kutoka kwa wakuu wa taasisi
mbalimbali za umma kwenda kwa maafisa na wafanyakazi wengine wote ni ule uliotolewa
Julai 25, 2016 na Kamishna wa TRA, Alphayo Kidata.
Kupitia waraka huo, wafanyakazi wote wa TRA wametakiwa kuwasilisha nakala za vyeti
vyao halisi kwa wakurugenzi wa utawala na rasilimali watu katika maeneo yao kufikia Agosti
15, 2016.
“Yeyote atakayeshindwa kutii agizo hili atawajibika mwenyewe,” inaeleza sehemu ya waraka
huo wa Kamishna wa TRA kwenda kwa wafanyakazi wote wa Mamlaka hiyo. Panga dhidi ya
watumishi waliogushi pia linatarajkiuwa kuwakumba watu walioomba kazi kupitia vyeti vya
watu wengine.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah
Kairuki, aliwahi kuiagiza Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu (Utumishi) kuwachukulia
hatua watumishi waliobainika kutumia vyeti visivyo vyao ili kupata ajira serikalini.
Wakati msako wa watumishi wenye vyeti bandia ukiendelea, Baraza la Mitihani Tanzania
(Necta), nalo lilitoa tamko zito lililowataka watu wote wanaojijua wazi kuwa wanamiliki vyeti
9/5/2016 Kimbunga vyeti feki chazoa vigogo kibao
http://www.ippmedia.com/sw/habari/kimbunga-vyeti-feki-chazoa-vigogo-kibao 4/5
0 Comments ippmedia.com 1 Login
⤤Share Sort by Best
Start the discussion…
Be the first to comment.
✉ Subscribe d Add Disqus to your site Add Disqus Add Privacy
Recommend
Magufuli ataka
Maalim Seif
akatwe posho,
auze nyanya
(/sw/habari/magufuliataka-maalimseif-akatweposho-auzenyanya)
Sumaye
akimbilia
mahakamani
(/sw/habari/sumayeakimbiliamahakamani)
Wenyeviti CUF
sasa wanena
mazito
(/sw/habari/wenyeviticuf-sasawanena-mazito)
Bilioni 100/-
zayeyuka Hazina
(/sw/habari/bilioni-
100-zayeyukahazina)
HABARI KUBWA
(Necta), nalo lilitoa tamko zito lililowataka watu wote wanaojijua wazi kuwa wanamiliki vyeti
bandia kujisalimisha wenyewe. Tamko hilo lilitolewa na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dk.
Charles Msonde, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
“Necta ndiyo yenye dhamana ya kutoa vyeti vyote vya watahiniwa wanaomaliza mitihani ya
Taifa nchini, kulikuwa na changamoto ya vyeti feki (bandia) kwa kipindi kirefu sasa
wanaojijua wajisalimishe maana watakamatwa tu,” alisema Dk. Msonde, akigusia tatizo la
kushamiri kwa vyeti bandia.
Prev (/sw/habari/tuzo-ya-jecha-yawakera-wanachama-wa-cuf-zbar)
Next (/sw/habari/magufuli-ataka-maalim-seif-akatwe-posho-auze-nyanya)
Jumatatu Septemba 05, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment