Gari likipita eneo hilo kwa tabu.
Mjumbe wa Mtaa wa Polisi Mabatini, jijini Dar es Salaam, Steven Jovin amesema kuwa barabara ya Kijitonyama (Polisi Mabatini) anaifananisha na sikio lisilosikia dawa kwa kuwa amelalamika sehemu mbalimbali hadi amecho.
Akizungumza na mwandishi wetu, Jovin alisema kuwa imekuwa kero kubwa ya muda mrefu kwa barabara hiyo ambayo ina dimbwi kubwa la maji pasipo kurekebishwa hali inayosababisha magari kupita kwenye makazi ya watu na kuharibu miundombinu ya maji na mazingira.
“Meya wa Manispaa ya Kinondoni alishafika eneo hili kuangalia lakini bado sijaona wakandalasi wakifika kutengenza barabara hii hasa eneo hili walau kwa kuweka vifusi,” alisema.
Akaongeza: “Kila siku vyombo vya habari vinakuja hapa kuchukua tukio hili sijui wahusika hawaoni jamani, naiomba watu wanaohusika waliangalie hili,” alisema Jovin.
NA DENIS MTIMA/GPL
No comments:
Post a Comment