Abiria Waaswa Kutoa Taarifa Kuhusu Madereva Wanaovunja Sheria

mpinga1-1

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi,  Hamadi Masauni akijiandaa kukata utepe kama ishara ya uzinduzi wa kampeni hiyo.
mpinga1-2…Akizungumza jambo katika hafla hiyo.
mpinga1-3Masauni na Mpinga wakitoa vipeperushi ndani ya moja ya mabasi ya kuelekea mikoani katika stendi ya Ubungo Dar.
mpinga1-4Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani , Naibu Kamishina wa Jeshi la Polisi (DCP), Mohamed Mpinga akiangalia mikanda ya kufunga abiria.
mpinga1-5Masauni alipotua stendi ya ubungo na kupokelewa na viongozi waratibu wa kampeni hiyo.
mpinga1-6Msanii wa Bongo Fleva, Tunda Man akitoa burudani kwa mashabiki wa muziki.
mpinga1-7Msanii wa Bongo Fleva, Tunda Man akitoa burudani kwa mashabiki wa muziki.
mpinga1-8Baadhi ya wananchi waliofika kwenye hafla hiyo.
mpinga1-9Masauni (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na waandaaji wa hafla hiyo.
KUELEKEA kipindi cha Sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya madereva wameaswa kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali na abiria kutoa taarifa kwa wanaokiuka sheria hizo kwa kutoa taarifa kwa wakati.
Hayo ameyasema leo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi,  Hamadi Masauni wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya ‘Paza Sauti’ iliyoratibiwa na Mabalozi wa Usalama Babarani RSA Tanzania katika Kituo cha mabasi ya mikoani Ubungo Dar.
Akifafanua alisema, kila mtu anawajibu wa kutoa taarifa dhidi ya dereva anayehatarisha maisha katika vyombo vya usafiri.
“Dereva kutokujua sheria za usalama barabarani isiwe kigezo cha kuvunja sheria zilizowekwa kwani waathirika wakubwa wa ajali ni Watanzania ambao ndiyo nguvu kazi ya kesho,”alisema Masauni.
Aidha aliendelea kufafanua kuwa, kampeni hiyo italeta matokeo chanya ambayo yataonyesha kupungua kwa ajali au kutokuwepo kabisa na kufanya Watanzania kuwa salama.
Naye Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Naibu Kamishina wa Jeshi la Polisi (DCP), Mohamed Mpinga amesema, kampeni iliyozinduliwa ni jitihada za kikosi cha usalama barabarani katika kupambana na ajali pamoja na kuongeza askari kila sehemu ambayo dereva wamekuwa wakikiuka sheria za usalama barabarani.
Amesema abiria wanatakiwa kuwa chachu ya kutoa taarifa za uvunjifu wa sheria za usalama barabarani kwa madereva ili waweze kuchukuliwa hatua kali.

No comments:

Post a Comment