Rais mstaafu wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete na Bw Chirau Ali Mwakwere Februari 2015.
Watumishi wa umma kikatiba wanafaa kujiuzulu kufikia 15 Februari.
Bw Mwakwere, ambaye mwishoni mwa wiki alitangaza rasmi kuhamia chama cha upinzani cha ODM, alikuwa awali mwanachama wa chama cha URP, moja ya vyama vilivyounda muungano wa Jubilee ulioshinda uchaguzi mkuu mwaka 2013.
Aliwania wadhifa wa seneta katika uchaguzi huo lakini akashindwa na Boy Juma Boy wa chama cha ODM.
Bw Mwakwere ni miongoni mwa waliotangaza nia ya kuwania wadhifa wa ugavana katika kaunti ya Kwale, baada ya gavana wa sasa Salim Mvurya kuhama chama cha ODM na kujiunga na chama Jubilee chake Rais Uhuru Kenyatta na Naibu Rais William Ruto.
No comments:
Post a Comment