Dar es Salaam. Jalada la kesi ya mauaji inayomkabili mjane wa bilionea Erasto Msuya, Miriam Mrita na Revocatus Muyela limeitishwa Mahakama Kuu.
Wakati jalada hilo likiitishwa Mahakama Kuu, kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilipaswa kutolewa uamuzi na Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa lakini ilishindikana kwa sababu hiyo, hivyo aliuahirisha hadi Februari 20.
Awali, Hakimu Mwambapa anayeisikiliza kesi hiyo alishindwa kutoa uamuzi kwa sababu kuna barua kutoka kwa ndugu wa marehemu Msuya iliwasilishwa mahakamani, hivyo alikuwa akisubiri maelekezo.
Kwa mujibu wa barua hiyo, wanataka hakimu huyo ajitoe kwa sababu hawana imani naye.
Hakimu Mwambapa alikuwa atoe uamuzi juu ya hoja zilizowasilishwa na upande wa utetezi na mashtaka.
Wakili John Malya aliomba washtakiwa waachiwe kwa madai hakuna hati ya mashtaka inayowashikilia, lakini Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa aliiomba mahakama iwape muda ili watekeleze amri iliyotolewa Januari 9.
No comments:
Post a Comment