VITA DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA, 80 WATIWA NGUVUNI ARUSHA

Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo akionyesha baadhi ya kete za Heroin ambazo zilikamatwa hivi karibuni kutokana na misako inayoenndelea mkoani hapa. (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)

Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
Wiki chache baada ya Jeshi la Polisi mkoani hapa kukamata gunia 58 za bhangi ambazo ziliteketezwa kwa moto  na kuharibu hekari 31 za mimea ya zao hilo katika maeneo ya Kismiri Juu na Engalaon wilayani Arumeru, Jeshi hilo limeendelea na misako dhidi ya wauzaji, watumiaji na wasafirishaji  wa dawa za kulevya na kufanikiwa kuwakata watuhumiwa 80 katika misako iliyofanyika kwa muda  wa siku 4 tu.

Akitoa taarifa hiyo leo asubuhi ofisini kwake mbele ya  waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo  alisema kwamba misako hiyo imefanikisha kukamata jumla ya kete 167 za madawa ya kulevya aina ya Heroin pia misokoto 3,845 ya Bhangi na mirungi kilogramu 33.

No comments:

Post a Comment