WAJAWAZITO,WATOTO KILOMBERO WAKOSA CHANJO KUTOKANA UMBALI WA VITUO VYA AFYA.


Wajawazito na watoto katika maeneo mengi ya wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro wamekosa huduma za msingi za chanjo na ushauri mwingine wa kiafya, huku kina mama wajawazito wakijifungua njiani na kupata matatizo mbalimbali ya uzazi, kutokana na umbali mrefu wa kuvifikia vituo vya afya na zahanati zinazotoa huduma hiyo.
Maria Mayanda ni mkazi wa kitongoji cha Mikochini Namawala B, kata ya Namawala wilayani Kilombero, ambaye ni miongoni mwa kina mama waliojifungulia njiani, kutokana na umbali wa zaidi ya kilometa 40 kufikia zahanati au kituo cha afya, ambaye anadai kupata tatizo hilo baada ya mito ya maeneo yao kufurika maji  nyakati za mvua na njia kushindwa kupitika kirahisi, hali iliyofanya viongozi wa maeneo hayo wakiongozwa na mwenyekiti wao matia nyambo,kuhamasishana na kujenga banda maalum kwaajili ya kupatiwa huduma za mkoba yaani mobile cliniki.

No comments:

Post a Comment