TUESDAY, MARCH 14, 2017
JALADA KESI YA NIDA LIPO KWA DPP
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeelezwa kuwa jalada la kesi ya uhujumu uchumi na kusababisha hasara ya bilioni 1.16 inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho (NIDA), Dickson Maimu na wenzake lipo kwa (DPP)
Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Leonard Swai, amesema kuwa, jalada hilo liko kwa DPP kwa ajili ya kufanyiwa tathmini ya upelelezi uliofanyika
Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage ameiahirisha kesi hiyo hadi Aprili 20,2017 kwa ajili ya kutajwa.
Maimu anashtakiwa pamoja na Meneja Biashara wa (NIDA), Avelin Momburi na Mkurugenzi wa TEHEMA, Joseph Makani.
Wengine ni Mhasibu Mkuu wa NIDA, Benjamin Mwakatumbula, Mkurugenzi wa Kampuni ya Aste Insurance Brokers, Astery Ndege, Ofisa Usafirishaji, George Ntalima, Mkurugenzi wa Sheria, Sabina Raymond na Xavery Kayombo.
Wanakabiliwa na tuhuma za kutumia madaraka vibaya, kula njama, kutumia nyaraka za uongo kumdanganya mwajiri na kuisababishia Serikali hasara ya milioni 1,169,352,931.
Maimu na Mwakatumbula wanadaiwa kutumia madaraka yao vibaya kati ya Januari 15 hadi 19, mwaka 2010 katika makao makuu ya NIDA wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Wanadaiwa kuidhinisha malipo kwa Gotham International Limited (GIL) ya Dola za Marekani 2,700,00 bila ya kutumia viwango vya kubadilisha fedha za kigeni vilivyowekwa na BOT.
Aidha wanadaiwa kuidhinisha malipo ya USD 1.8 kwa GIL bila kuzingatia viwanjo vya fedha.
Ilidaiwa kuwa, Juni 20, 2014, waliidhinisha USD 675,000 kwa GIL bila ya kuzingatia viwango vya kubadilisha fedha, hivyo kuifanya kampuni hiyo kupata faida ya Sh 42,471,000.
Post a Comment