KUJITOLEA KUFUNDISHA KISWAHILI

OTSONYA MSAFIRI,                                     
CHUO KIKUU DAR ES SALAAM,
                                             S.L.P 35091,
                                                          DAR ES SALAAM.
                                           28/04/2015.
LUKE JOE,
VIJIMAMBO.
Ndugu,
            YAH: KUJITOLEA KUFUNDISHA KISWAHILI ZA NJE.
Husika na mada tajwa hapo juu, Naitwa Otonya Msafiri, Mtanzania mwenye umri wa miaka 23. Mimi ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika Chuo kikuu Dar es salaam ninayetarajia kuhitimu masomo yangu mwezi wa sita mwaka huu. Ninasomea shahada ya sanaa na elimu katika somo la Kiswahili pamoja na Fasihi kwa kingereza (Literature). Nina maendeleo mazuri kiitaaluma kwani kwa mwaka wa kwanza nimefanikiwa kupata G.P.A ya 4.1 na mwaka wa pili nimefanikiwa kupata G.P.A ya 4.4. hata hivyo, natarajia matokeo mazuri kwa mwaka huu wa mwisho.
Aidha, kwa nia ya dhati kabisa napenda kuomba nafasi ya kufundisha Kiswahili kwa wapenzi wa lugha hii nchini Scotland kwa sababu za msingi nne; kwanza ni ndoto yangu ya kueneza tamaduni zetu ulimwenguni kote na hii ni pamoja na kueneza lugha yetu pendwa ya Kiswahili. Pili, napenda kujifunza tamaduni zingine ili kuweza kubaini mabadiliko yanayoweza kuleta athari chanya kwa jamii zetu, tatu, napenda kutumia maarifa yangu kwa maslahi mapana ya jamii inayonizunguka na mwisho ni kutafuta fursa zozote za kitaaluma ndani na nje ya Tanzania ili kuweza kujimudu kimaisha mimi pamoja na wote wanaonitegemea.
Hivyo basi, kwa heshima na taadhima, naomba uchukue ombi langu kwa jicho pevu, ili kunifanikisha fursa yoyote inayoendana na taaluma yangu kwa maslahi mapana ya nchi yangu pamoja na ulimwengu kwa ujumla. Napenda kuambatanisha vivuli vya vyeti vyangu pamoja na wasifu wangu kwa ufafanuzi zaidi. Natarajia jibu zuri mara baada ya kupitia nakala zangu na kujiridhisha.
Wako katika ujenzi wa taifa letu la Tanzania,
Otonya Msafiri  
WASIFU BINAFSI
MAELEZO BINAFSI
JINA: Otonya Msafiri      
BARUA PEPE: Otonyam@gmail.com
ANWANI YA KUDUMU: S.L.P 59, Shirati Rorya
JINSIA: Me.
NAMBARI ZA SIMU: 255759045608
ELIMU
Mimi ni mwanafunzi wa shahada ya kwanza katika Chuo kikuu Dar es salaam katika fani ya sanaa na elimu (BAED) kwa masomo ya Kiswahili na Fasihi kwa kingereza (Literature). Natarajia kuhitimu mwezi wa sita mwaka huu (2017). Matokeo yangu kwa mwaka wa kwanza ni G.P.A ya 4.1 na mwaka wa pili ni G.P.A ya 4.4

No comments:

Post a Comment