Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Programu ya Maendeleo (United Nations Development Programs – UNDP), Bi. Awa Dabo aliyeondolewa nchini.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeliagiza Shirika la Umoja wa Mataifa la Programu ya Maendeleo (United Nations Development Programs – UNDP) kwa upande wa Tanzania kumuondoa nchini Mkurugenzi wa Shirika hilo Bi. Awa Dabo.
Serikali ilifikia uamuzi huo kutokana na Bi. Dabo kutokuwa na maelewano mazuri na baadhi ya Watumishi wenzake na Menejimenti ya Shirika hilo, hivyo kupelekea kuzoretesha utendaji wa shirika hilo nchini na kupunguza kasi ya kuleta maendeleo kwa Watanzania endapo hatua za haraka zisingechukuliwa.
No comments:
Post a Comment