Baadhi ya wananchi wa Kata ya Olasiti kama wanavyoonekana pichani.Picha na Vero Ignatus blog.
Na .Vero Ignatus,Arusha.
WAKAZI wa Olasiti jijini Arusha wamesusia maji yanayotolewa na Idara ya maji na kudai kuwa maji hayo hayafai kwa matumizi ya aina yoyote.
Wakizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanywa na mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo wananchi hao walisema maji yaliyosambazwa na Idara ya maji yana chumvi kiasi cha kuharibu hata mimea wanapojaribu kumwagilia.
Mmoja wa wakazi hao Meck Mollel alisema wanahofia baada ya miaka ijayo kutokuwa na nguvu za kiume kutokana na kuendelea kutumia maji hayo ambayo yanaladha ya magadi.
"Kweli haya maji yanatupa hofu baadaye tutajikuta wanawake wote kwa mpango huu hatuyahitaji haya maji tuleteeni maji yaliyorafiki kwa binadamu" alisema Mollel.
No comments:
Post a Comment